RASMI uongozi wa Geita Gold umemalizana na aliyekuwa nyota wa Yanga, Saido Ntibazonkiza kwa mkataba wa miaka miwili.

Ntibazonkiza alimaliza mkataba wake na Yanga mwishoni mwa msimu uliopita ambapo timu hiyo chini ya Kocha Mkuu, Nassredine Nabi haikumuongezea mkataba.

Saido Ntibazonkiza, Saido Ntibazonkiza Alamba Mkataba Geita Gold wa Miaka 2, Meridianbet

Akizungumzia usajili huo, Ofisa Habari wa Geita Gold, Hemed Kivuyo amesema kuwa “Ni kweli tumemalizana na Saido kwa mkataba wa miaka miwili.

“Tumechelewa kumtangaza kutokana na makubaliano ya muda mrefu tuliyokuwa nayo ambapo hatukuafikiana lakini kwa sasa ni mchezaji wetu.” 

Kutokana na uzoefu mkubwa alionao Saido kwenye mashindano mbalimbali utaisaidia Geita Gold hasa kwenye michuano ya Shirikisho barani Afrika ambapo timu hiyo itashiriki.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa