Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amekanusha kuwa uchovu unaweza kuwa kikwazo kwa yeye na wachezaji kutofanya vizuri lakini amewataka wachezaji wake kushuruku kwa kubaki kushindania makombe matatu.

Man City siku ya jumatano wanakutana na ATL Madrid kwenye mchezo wa pili wa ligi ya mabingwa ulaya, siku mbili tu baada ya kutoka kwenye mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Liverpool.

Pep Guardiola

Pep Guardiola wakati akiwa anahojiwa na waandishi wa habari alinukuliwa akisema, “inapaswa kushukuru kuwa hapa, mchezo huu, mwingine, mwingine, ni kwa sababu tumefanya vizuri mpaka sasa, kwa kipindi hiki huwezi kuchoka, unaweza kupoteza kwa sababu umecheza vibaya au mpinzani wako ni bora zaidi yako sio kwa sababu ya uchovu.

“Tumesafiri mpka Madrid tukiwa na matokea mazuri, pia tumekuja kwa kusudi la kuhitaji ushindi, tutajaribu kutafuta goli ndani ya dakika 5-10 ikiwezekana, haitakuwa rahisi, kwa sababu wako nyumbani, watakuwa hatabiriki na kuna muda wataukuwa wanashambulia sana, itatupasa kuzoe na kujilinda zaidi kwa muda.”

Baada ya kumalizana na Atletico Madrid kwenye mchezo wa robo fainali ya ligi ya mabinwa Ulaya kesho, kikosi cha Pep Guardiola kinataraji kucheza mchezo wa nusu fainali ya kombe la FA Cup dhidi ya Liverpool, siku tano baada ya kukutana kwenye mchezo wa kigi kuu ya uingereza ambapo walitoka sare ya 2-2.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa