UEFA Kufanya Mabadaliko ya Sheria ya "Financial Fair Play"

Shirikisho la mpira wa miguu ulaya UEFA  siku ya alhamisi watatangaza mabadiliko ya sheria za “Financial Fair Play” ili kubadilisha mbinu za mpira wa ulaya  kutokana na klabu nyingi kutetereka kutokana mlipuko wa uviko-19 na kutokuwa na usawa matumizi ya pesa.

Baada ya mazungumzo ya mwezi mzima, UEFA wanatarajia kufanya mabadiliko makubwa ya mfumo mzima wa sheria ya “Financial Fair Play” (FFP) ulioanzishwa mwaka 2010 ili kuzuia klabu kuingia kwenye madeni wakati wakiwa kwenye kinyanganyiro cha kutafuta ubingwa.

UEFA itajikita kwenye mabadiliko ambayo itahitaji klabu zote kuweka mlinganyo sawa wa kifedha ili kuzuia matumizi ya mishahara, ada za uhamisho na ada za mawakala.

Njia ya hii mabadiliko itazifanya klabu zivutie wawekezaji kwa kuwekeza pkiasi cha pesa chenye ukomo, Raffaele Poli, mkurugenzi wa CIES soccer observatory alinukuliwa akisema.

“Unaweza kuingiza pesa nyingine, lakini huwezi kuozipoteza zote kwenye kuajiri na kulipa mishahara, hata klabu kubwa bado ni wahanga wa mfumuko wa mishaha mikubwa.”

Kwa miaka 12 “Financial Fair Play” (FFP) imekuwa ikihakikisha akaunti zote za klabu ziko sawa na ukomo wa matumizi uko sawa na safi.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe