Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Roberto Firmino raia wa Brazil  ameonesha kusikitishwa kuachwa kwenye timu ya taifa ya Brazil ambayo itakwenda kushiriki michuano ya kombe la dunia nchini Qatar.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram Firmino alieleza namna ambavyo amesikitishwa na yeye kuachwa kwenye timu hiyo, Kwani kila siku amekua akijiskia fahari kuiwakilisha timu hiyo kwani ana mapenzi makubwa na taifa lake.firminoMshambuliaji huyo ameweka wazi kua mambo yameenda tofauti ambavyo alitarajia kuitwa kwenye timu hiyo, Lakini hakufanikiwa kuitwa kwenye timu hiyo cha zaidi amemshukuru mungu na kuwapongeza ambao wamechaguliwa kuliwakilisha taifa hilo.

Siku ya Jumatatu saa moja kamili usiku kwa saa za Afrika mashariki kocha wa timu ya taifa ya Brazil Tite alitangaza kikosi cha timu ya taifa hilo ambacho kitaiwakilisha Brazil kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Qatar.firminoLakini jambo la kushangaza ni kukosekana Roberto Firmino ambae watu wengi pia wameshtushwa kutokana na jambo hilo kutokea, Huku wengi wakiamini mshambualiaji huyo alistahili kuingia kwenye kikosi hicho na kwenda kuliwakilisha taifa hilo nchini Qatar.

AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa