Ten Hag: Tutaingia Sokoni Januari Kutafuta Mshambuliaji

Kocha wa klabu ya Manchester United Eric Ten Hag ameweka wazi kua wataingia sokoni kwenye dirisha dogo mwezi Januari kutafuta mshambualiaji ili kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo.

Klabu ya Manchester United inataka kuongeza mshambuliaji baada ya kuondokewa na mchezaji wake nyota Cristiano Ronaldo ambaye alitangaza kuondoka klabuni hapo wiki kadhaa zilizopita, Hivo klabu hiyo inahitaji mshambuliaji ili kuongeza nguvu katika safu yao ya ushambuliaji.ten hagKocha wa Manchester United Ten Hag amesema ni kweli wanahitaji mshambuliaji lakini lazima wapate mchezaji sahihi na kusisitiza watafanya kila kitu kwenye nguvu yao kuhakikisha wanapata mshambuliaji wa maana katika eneo hilo.

Kocha huyo pia ameleza watafanya uchunguzi katika kila furasa itakayopatikana ya kupata mshambuliaji ndani ya timu hiyo katika majira ya baridi, klabu hiyo imekua ikiteseka kwenye nafasi ya mshambuliaji kwa kipindi cha muda mrefu sasa.ten hagManchester United wanahitaji mshambuliaji kwa kila namna kwakua mshambuliaji pekee mwenye asili ya kucheza eneo la katikati kwenye timu hiyo ni Anthony Martial ambaye anaonekana kuimarika chini ya Ten Hag, Lakini shida kubwa ya mchezaji huyo ni kupata majeraha ya mara kwa mara.

Acha ujumbe