BAADA ya kukosekana kwenye mchezo uliopita wa ligi kuu dhidi Ruvu Shooting, nyota wa Yanga, Stephane Aziz ki ameongeza mzuka kwenye kambi ya Yanga baada ya kujiunga na kambi hiyo.

Kwenye mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar jumatatu Yanga walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 yakifungwa na Bakari Mwamnyeto na Feisal Salum.

Yanga ambayo imeweka kambi kwenye kijiji cha Avic kilichopo Kigamboni, Dar kinajiandaa na mchezo wao wa kimataifa dhidi ya Al Hilal ya Sudan.

Akizungumzia maandalizi yao, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa hali ya kambi yao ipo salama na kila kitu kinaenda kama kilivyopangwa.

“Kila kitu kipo sawa kuanzia kwenye uongozi, benchi la ufundi huku pia wachezaji wakiendelea na maandalizi kuelekea katika huo mchezo.

“Ni kweli Aziz Ki amejiunga na wenzake baada ya kurejea kutoka kwenye majukumu ya timu ya taifa na amejiunga moja kwa moja na timu kwa ajili ya kuhakikisha anaenda kuipambania nembo ya timu ya Yanga kwenye michuano ya kimataifa.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa