Kwenye mashindano hayo ya Mbeya Super Cup ambayo yanafanyika mkoani Mbeya tayari Ihefu wamecheza mechi moja dhidi ya Mbeya City na kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Akizungumzia hilo Katwila amesema “Tunamshukuru Mungu kikosi kipo salama kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao wa ligi.
“Kesho tunatarajia kucheza mechi ya pili ya mashindano ya Mbeya Super Cup na haya mashindano tunayatumia kwa ajili ya maandalizi ya michezo yetu ya ligi.
“Kikosi kwa sasa kinaonekana kuwa na muunganiko kwani hata wachezaji ambao tumewasajili wana uzoefu hivyo tuna imani watatusaidia.”

