Staa wa klabu ya Manchester United Mason Greenwood leo ameachiwa kwa dhamana kutoka na kesi yake inayomkabili ya kufanya jaribio la ubakaji.
Mchezaji huyo ambaye ameshikiliwa toka mwezi Januari mwaka huu kwa kosa la kufanya jaribio la ubakaji kutokana na video zilizoibuka mitandaoni na kufanya mchezaji huyo kutiwa hatiani na mpaka leo hajafanikiwa kurudi uwanjani.
Mchezaji huyo ambaye alipandishwa kizimbani siku ya jumatatu na kubaki rumande mpaka leo jumatano baada ya kesi hiyo kusikilizwa faragha hatimae Greenwood amefanikiwa kupata dhamana.
Baada ya kuachiwa leo hii Mason Greenwood amepewa masharti baada ya kuachiwa kwa dhamana leo hii mahakama imemtaka mchezaji kutokuwasiliana na mashahidi ikiwemo mlalamishi pamoja na kuishi kwenye Anwani ya Bowdon sehemu anayoishi.
Kijana huyo mwenye miaka 21 alianza kutabiriwa makubwa kutokana na ubora ambao alikua anauonesha uwanjani lakini wadau wa soka walisikitishwa na kitendo ambacho alikifanya mchezaji huyo kijana ambacho mpaka sasa kimeeka hatiani hatma ya maisha yake ya soka.

