Nyota wa klabu wa inayopatika kati ya mtaa wa twiga na jangwani wameajianda na mchezo ujao wa ligi dhidi ya Simba, baadhi ya nyota wa kikosi cha Yanga wameahidi kupata ushindi kwenye mchezo huo.
Mtanange huo ambao ni dabi ya kariakoo unaoteka hisia za watu mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania utapigwa Oktoba 23 mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Yanga wanashuka kwenye mchezo huo wakiwa na pointi 13 sawa na vinara Simba huku tofauti ikiwa ni idadi ya mabao ya kufungwa na kufunga.
Akizungumzia maandalizi yao, kiungo wa Yanga, Zawadi Mauya amesema “Tunaendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Simba.
“Utakuwa mchezo mgumu lakini tutaingia kupambana kwa ajili ya kuhakikisha tunaibuka na ushindi kwenye mchezo huo.”

