Ancelotti Ampongeza Vinicius

Kocha wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti amempongeza mchezaji wake Vinicius Jr ambaye ameonesha kiwango cha kipekee katika mchezo wa jana dhidi ya klabu ya Osasuna kwenye mchezo wa ligi kuu ya Hispania.

Carlo Ancelotti anamuona Vinicius Jr ni kama ameziba pengo la Karim Benzema ambaye alikosekana katika mchezo wa jana dhidi ya Osasuna, Lakini winga huyo wa kimataifa wa Brazil alikua kwenye kiwango bora sana na kuisaidia klabu yake kupata matokeo ya ushindi.ancelottiMshambuliaji Karim Benzema alipumzishwa katika mchezo wa jana wa ligi kuu ya Hispania dhidi ya klabu ya Osasuna, Huku winga wa kimataifa wa Brazil akifanya vyema zaidi katika mchezo wakiwa ugenini na kufanikiwa kupunguza pengo la alama mpaka kufikia tano kutoka kwa vinara wa ligi kuu nchini humo klabu ya Barcelona.

Ancelotti baada ya mchezo alimzungumzia Vinicius kwa kusema “Ni wazi Vinicius ameleta mabadiliko, Alikua na mchezo mzuri, ni mchezaji wa ajabu” Ameyazungumza hayo kocha huyo baada ya mchezo wa Real Madrid uliopigwa katika dmba la El Sadr dhidi ya Osasuna.ancelottiKlabu ya Real Madrid jana walimpumzisha nyota Karim Benzema katika mchezo wa ligi kuu ya Hispania, Ikiwa inatafsiriwa kocha Ancelotti alifanya hivo makusudi kwajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi ya mabingw aulaya hatua ya 16 bora dhidi ya klabu ya Liverpool utakaopigwa katika dimba la Anfield siku ya jumanne.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.