Barcola Nje Wiki Kadhaa Baada ya Kuumia Kifundo cha Mguu

Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Bradley Barcola, anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa wiki kadhaa baada ya kupata jeraha baya la kifundo cha mguu wa kulia wakati wa mchezo wa UEFA Champions League dhidi ya Chelsea uliochezwa jijini London.

Barcola Nje Wiki Kadhaa Baada ya Kuumia Kifundo cha MguuKwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo ya Ufaransa, Barcola alipata majeraha ya mishipa (ligaments) kwenye kifundo cha mguu, hali iliyomlazimu kutolewa nje dakika ya 59 ya mchezo na nafasi yake kuchukuliwa na Desire Doue.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Katika mchezo huo, PSG iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Chelsea, na kufuzu hatua ya robo fainali kwa jumla ya mabao 8-2. Barcola alifanikiwa kufunga bao la pili katika ushindi huo muhimu.

Barcola Nje Wiki Kadhaa Baada ya Kuumia Kifundo cha MguuBaada ya ushindi huo, PSG sasa inakutana na Liverpool katika hatua ya robo fainali, huku mchezo wa kwanza ukitarajiwa kuchezwa Aprili 7 au 8.

Jeraha hilo pia linatarajiwa kumuweka nje Barcola kwenye michezo ya kirafiki ya timu ya taifa ya France dhidi ya Brazil na Colombia itakayochezwa wiki ijayo.

Barcola Nje Wiki Kadhaa Baada ya Kuumia Kifundo cha MguuBarcola mwenye umri wa miaka 23 ni miongoni mwa wachezaji muhimu wa PSG msimu huu, hivyo kukosekana kwake ni pigo kwa klabu hiyo na timu ya taifa ya Ufaransa kuelekea michezo ijayo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.