Ule msemo wa “yametimia” umeweza kudhihirika uwanja wa taifa Tanzania pale ambapo timu ya taifa ilipowasambaratisha Waganda katika ardhi yao. Ni aina ya mechi iliyovutia na iliyojaa shamrashamra na hamasa ya kutosha. Ni jambo la kheri kwa taifa hilo kupeleka wawakilishi wawili kimataifa kwa siku za hivi karibuni.
Yalikuwa ni maombi ya kila mmoja kutaka timu hiyo kutinga hatua hiyo muhimu ili kuweza kuvunja uteja wao wa kushiriki mashindano makubwa ambayo kwa miaka mingi wamekuwa wakitolewa mapema sana na kuwafanya kuonekana kama timu ambayo haipo kiushindani kabisa wakiwa wamewaadhibu The Cranes 3-1.
Hawakuwa na sababu ya kupoteza mechi hiyo kutokana na mgeni wao Uganda kuwa tayari amekwisha kata tiketi ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo kwa alama zake 13 na alikuwa anaendelea kushikilia kundi hilo na Taifa Stars wanafuatia kwenye kundi hilo baada ya kushinda mechi hiyo.

Ni ushindi wa kishindo kwa taifa hili kwa sababu hawana historia nzuri kufanya vizuri kwenye michuano hiyo. Kwa sasa wanaonekana kuonesha ukomavu wa aina yake baada ya kushinda mechi hiyo na kutinga hatua inayofuata kwenye michuano. Ni hatua ngumu sana lakini hawana budi kugangamala ili kufanya vizuri zaidi.
Ni jambo lisilopingika na lenye ufahari kwa nchi, hasa nchi kama hizi ambazo mara nyingi zimekuwa zikikosa ushiriki wa michuano hii mikubwa; japo wameonesha mabadiliko na hatua kubwa sana kuudhihirishia ulimwengu kwamba nao wapo japo wanakosa nafasi ya kuwika tu.
Hizi sasa huwa ni nyakati muafaka kwa wachezaji kutambulika kimataifa na kupata nafasi ya kuonesha uwakilishi wao kimataifa lakini baada ya ushindi huo ni imani kwamba ulimwengu mzima umetambua uwepo wa taifa hili kisoka na kutambua uwezo wa wachezaji iwe kwa timu nzima na kwa mchezaji mmoja mmoja.

Sio timu hiyo pekee imeweza kufanya vizuri kwenye michuano hiyo mikubwa bali zipo timu nyingine pia kama Simba ambazo ni wawakilishi wakubwa kwenye michuano hiyo na wanaliwakilisha taifa kimataifa. Pia, kwa upande wa masumbwi wameonesha uwakilishi wao kupitia Hassan Mwakinyo aliyefanya makubwa ya kulifurahisha taifa lake. Wachezaji wanapotumia nafasi zao kama hivi hukuza hadhi zao na kupandisha thamani za taifa husika kwa kipindi husika.
Tunawapa nafasi ya kuweza kufanya vizuri zaidi kwenye michuano hiyo kutokana na ukomavu waliounesha kwenye mechi hiyo. Japo wanakoendelea wanahitaji ukomavu zaidi ya hapo maana aina ya timu anazoenda kukutana nazo zina uzoefu maradufu. Pia, mashabiki washukuriwe kwa kuonesha uhalisia wa kile walichokifanya katika kuipa nguvu timu yao.


Povel
Habar njema