Makala mpya inayomuhusu Sadio Mane iliyo tengenezwa nchini kwao Senegal inayo muhusu mchezaj huyo wa Senegal na Liverpool imeachiwa leo bure na Rakuten TV. Makala hii inatuonesha ni kwa jinsi gani maisha yalikua kabla ya Mane kufikia hapo alipo sasa. Historia hiyo imegusa mambo mengi sana ila kwa sasa tuangalie mambo matano makubwa ya kujifunza kutoka kwa Mane.
- Mane ilibidi akimbie nyumbani kwao ili akacheze mpira.
Yawezekana unaijua hii ya Sadio Mane kutoroka nyumbani lakini kwa kijana mdogo aliyekulia kwenye kijiji kidogo kinachoitwa Bambali huko Senegal, familia ya Sadio mane haikuamini kabisa kama mpira ungeweza kumsaidia kuishi, Baba mzazi wa Sadio Mane alifariki Mane akiwa na umri wa miaka 7 tu na hilo likapelekea Mane kulelewa na kaka wa Mama yake, Ambaye alikua ni kuingozi wa kidini kwenye kijiji cha Bambali ambapo kwa mjomba huyo elimu kwa Sadio Mane ndio ilikua kila kitu
“mjomba wangu hakutaka nicheze mpira kwasababu aliamini elimu ni muhimu Zaidi, ila mambo yakaenda tofauti na hakupenda kabisa” Mane alisema
Mwaka 2008 Mane alipofikia miaka 16 akakimbia Dakar ambako ni mji mkuu wa Senegal kwa siri ili akajaribu kuingia kwenye timu huko, Aka kamatwa na kurudishwa nyumbani na akawaahidi kua mwaka unaofuata hatosoma tena ita kua yeye na mpira, mpira nayeye.
- Alitamani sana kua kama EL Hadji Diouf

Sadio Mane alikua na miaka 10 tu wakati Senegal inafika robo fainali ya mashindano ya kombe lamataifa ya Africa ambayo ilihusisha wakongwe kama Aliou Cisse, Khalilou Fadiga na El Hadji Diouf.
“kile ndio kilikua kipindi bora Zaidi kwenye historia ya soka la Senegal” Mane alisema
Wapo wanaosema Mane ameshafikia rekodi za shujaa wake Diouf angalau kwa kuitumikia Liverpool. Ametengeneza historia nzuri Zaidi akiwa na Liverpool kuliko shujaa wake.
- Hali ya hewa ya Ulaya ilimtesa
Mane alipotoka Senegal kwenda Ufaransa alijiunga na timu ya Metz mwaka 2011. Na kitu pekee alicho kipitia na kikampa wakati mgumu kwa mwezi January kule Ufaransa ni baridi. Mane alielezea jinsi wachezaji wenzake walivyo mshangaa baada ya kutoka na Sweta kwenye chumba cha kubadirishia nguo “walianza kucheka na sikujua wanacheka nini “ ikabidi awaulize “waka niambia inakuaje unavaa hivyo?”
Mane anasema kipindi alichokipitia FC Metz ndio kimemfanya kua Mane tunae muona leo, Mwanzoni mwa utumishi wake pale Metz alipatwa na tatizo la nyonga ila hakuwahi kumwambia mtu yeyote kwasababu ya kuhofia kurudishwa Senegal.
Miezi 8 baadae akapata matibabu na kupona kabisa na kilichofuata ni historia.
- Mane hakuaminiwa kabisa na Jurgen Klopp

Kaika kila kipande ambacho Klopp alizungumza kwenye Makala hiyo, Clopp alizungumzia namna alivyo mtafsiri vibaya Mane mara tu alivyo tambulishwa kwake.
“alionekana mdogo sana amekaa mbele yangu na kofia yake ya Baseball pamoja na dawa kidogo aliyoweka kwenye nywele zake ambazo mpaka sasa hivi nadhani bado anaweka alionekana kama mwanamuziki anaechipukia nikasema sitakua na mda na mtu wa namna hii”
Klopp mpaka sasa hivi anajutia namna alivyo mtafsiri Mane vibaya “mi ni mtu mzuri sana kwa watu ila kwa hili nilikosea mno”
- Mashabiki wa nyumbani ni wagumu Zaidi kuliko wa huko aliko

Sadio mane anawakubali sana mashabiki wa nyumbani kwao kwa maana ya timu ya taifa ya Senegal. Kwasababu wanampa changamoto sana mashabiki wengi wanasema Mane anafanya vizuri Zaidi kwenye klabu yake kuliko timu ya taifa huku wengine wakisema kua kwasasa Mane ndie mchezaji bora wa kipindi chake kutokea Afrika lakini maajabu yake hatuyaoni nyumbani, Mane amejenga nyumba kwa ajili ya wajomba zake na kujenga Hospitali za wilaya katika nchi yake. Ni wazi kua ni mfano wa kuigwa.
Vipo vingi vya kujifunza kwa Mane ila hayo ndio machache kati hayo mengi uliyopaswa kuyajua kutoka kwa Sadio Mane.


aisha
Mane ni mpambani sana
Zeiyana
Makala nzuri sana nilikua sijui vingi kuusu mane daah..! ukisimamia ndoto zako unafika mbali