Sasa usiku wa pambano hilo Ali hakujua kama ana shabiki yake anamtazama usiku ule ambae ni Mike Tyson .Wakati Ali amekula kipondo cha kutosha na corner yake kutupa taulo uwanjani, kila mtu aliteseka sana na kipigo kile, ila mitaa ya New York kijana Mike Tyson na miaka yake 14 alilia zaidi kuliko mtu yoyote

Mwalimu wake Cus D’Amato aligundua mateso ya Mwanafunzi wake, asubuhi sana alimpigia Ali na kumwambia kuna mtoto mdogo sana anahitaji kuongea na wewe, Tyson alivyopewa simu “Nitalipa juu ya fedheha uliopata” ni maneno pekee Mike aliahidi Asubuhi ile ya October 3,1980
Cus D’Amato alitamani mtoto yule atimize ndoto yake, alitamani mtoto yule kutoka mitaa ya wababe na makundi ya kihuni ya New York atimize ahadi ya Ali, ilikua mazoezi ya usiku na mchana, jasho likimtoka kuelekea kupanda mlima wa Sayuni ya Ndondi
Bahati mbaya sana shahidi wa ndoto ile Cus alitangulia mbele za haki, alibaki Tyson na Ali pekee wanaikumbuka ahadi ile, Tyson anabeba ubingwa wa dunia 1986 akiwa na umri mdogo wa miaka 20 tu lakini hakufurahia kwakua Mwalimu wake katangulia kaburini, hakufurahia kwakua bado hajatekeleza ahadi ya Ali
Larry Holmes aliwa tayari amestaafu ndondi ila Tyson alimuhitaji Holmes uwanjani kwenye pambano la kisasi kwakua alimtesa Role model wake, alitumika Promoter Don King kulazimisha sana Holmes wa miaka 38 arejee ulingoni, baada ya dau kubwa sana Holmes alikubali kurejea tangu apoteze dhidi ya Michael Spinks
https://www.youtube.com/watch?v=fjbaoQ-P8ww
January 22,1988 ndipo walipanga kupanda ulingoni, likapewa jina la World Heavyweight History, kama Holmes angeshinda angekuwa bondia wa nne kutwaa mkanda huo baada ya kuupoteza kama Floyd Patterson, Muhammad Ali na Tin Witherspoon, aliitamani sana rekodi hiyo bila kujua akili ya Tyson
Kabla ya pambano kuanza Ali alikuwepo pale Trump Plaza New Jersey, alimfuata Tyson na kumwambia “Unakumbuka ahadi yako ukiwa bado mdogo??” Mike alicheka kisha akajibu nakumbuka Master, kilichotokea baada ya kengele hakuna alietarajia
Mike hakukamatika anadance, anatupa na anajilinda, Holmes kila muda anamkumbati, aalianguka mara mbili Holmes ila jab ya tatu ilimpeleka chini na Refa Joe Cortez alimpa ushindi Tyson kwa TKO, hatimae alitimiza ahadi yake kwa Mpendwa wake


Aziza mushi
Asanteni kwa habari meridianbet.
Warda
huu ndo ulikuwa mwanzo wa kumjua Tyson #Meridianbettz
Samiah
Meridianbet asanteni kwa taarifa
Tahiya
Tyson alitimiza ahadi yke kwa Mohamed Ally wamarekani weusi mwenye rekodi nzur kwnye masumbwi
Mariam mtandama
Meridianbet muko vizur
Salma
Nia yake na ahadi yake vilimfikisha mbali mike T
Hope mwaikuka
Hii mpya kwang axanten sana
Rehema
Hii ni bonge la makala asnte sn meridianbet kw makala mzuri sn
Elika
Mohamed ally alikuwa na kipaji sana
Sadick
Unasikia majina Mike Tyson na Mohammed Alli kitu pekee kinachokujia kichwani ni ndondi#meridianbettz
Frank Patrick
Ahadi iliyotimizwa…mike iron
Agness
Asante kwa taarifa meridian
Genia Sikaluzwe
Mike ametimiza ahadi ambayo aliiweka kwa Muhammad Ali,alitembea na ahadi kichwani
Neema hassan
Asante kwa habari za michezo na burudan#meridianbettz
Antony Luseno
Nyakati alizokuwa akipanda ulingoni lazima utamani kushuhudia pamabano lake
Theckla
Pongezi kwa Mike kutimiza ahadi yake kwa master wake
Ester mmakasa
Mike Tyson alikuwa mbavu kwakweli miaka iyo sijui nani atachukuwa nafasi yake tena.
Adelta
Good news# meridianbet
Rehema Dickson
Asante kwa habar sikulijua hili swala shukran kwa taarifa
winfrida
historia nzuri sana kwetu sisi mashabiki wa ngumi
julieth boniface
big up very interesting story
David Pere
Mohamed Ally ni bondia hatari Sana kwa wakati wake maana hata Tyson mwenyewe alichemka kupogana naye
Isaya massawe
Aliweka juhudi katika kutimiza kile alichodhamiria
mwakalosi
king of dancing in rings
Asha mvugalo
Thnks meridian bet tz kwa update za michezo na burudani
JULIANA
Kumbe Tyson alipenda ndondi akiwa mdogo,
Emmy cleopa
Ahsante meridian kwa taarifa
Ernest
Ali na Tyson walikuwa noumer sana kuwadondosha
Gabriel
Kwel ndo huwa kwel
Dorophina
Makala nzuri sana hii
Lydia Emmanuel Magoti
Walikuwa noma Sana yani nawakubali wapiganaji hao
Caroline
Aiseee mpambano ulikua motooo
lombo
cpat picha iyo siku tyson alikuwa makin sana asiabike yy pamoja na master wake
Povel
Tyson for me alikuwah Bora sana kpnd chake thnks meridian bet kwa update za michezo
Furahav
Ilikuwa hatari sana.
mathayo sonje
Hizi ndio ndoto tunatakiwa tuziote, meridianbet wanatufundisha vitu safi sana, huku tunafurahia kupata pesa huku tunapata na elimu pia.#meridianbet
Theonestina
Enzi izo Tyson alikuwa gumzo dunian
Hidaya
Mmenijuza kitu ambacho sikuwahi kukifahamu kuhusu Tyson asante meridianbet
Evaluziga
Huu ndio mwanzo wa kumjua tyson
Ester jackson
Hii ni history ya kusisimua asante meridian kwa kutupa habari motomoto za michezo
Neema juma
Waooo Mike Tyson kaacha historia nzuri ya kukumbukwa na wengi
Kenani
Mwenye mikono take ya dhaabu mkono wa bahat amewika Sana ulingoni hyu jamaa