Mchezaji wa kikapu kutoka timu ya Indiana Pacers Malcolm Brogdon amethibitishwa kupimwa na kukutwa na Virusi vya Korona.

Brodgon mwenye umri wa miaka 27 amekuwa akionesha jitihada za kupigania haki za usawa kwenye jamii tangu kuzuka kwa janga la Korona mwezi machi hivyo kupelekea shughuli nyingi kusimama.
Msimu wa NBA 2019-20 unatarajia kurudi katika viwanja vya Disney World katika mji wa orlando mwashoni mwa mwezi julai, na wachezaji wameripotiwa kuanza kujinoa kwenye vituo vyao wiki hii.
“Hivi karibuni nilipima na nimepatikana na maambukizi ya Virusi vya Korona kwa sasa nipo karantini,” Brogdon alisema.
“Naendelea vizuri, na ninatarajia kujiunga na wachezaji wenzangu mwishoni mwa mwezi julai kwaajili ya kuendelea na msimu wa NBA kwa michezo ya awali.”
Brogdon alijiunga na Indiana Pacers akitokea Milwaukee Bucks mwaka 2019 na huu ndio msimu wake wa kwanza akiwa na Indiana Pacers. Pia Brogdon alikuwa nje ya kikosi kutokana na majeraha kabla ya ligi kusimama mwezi machi, lakini mwezi Aprili ilielezwa kuwa yupo sawa kiafya kwa “100%.”
Pacers wamepanga kutua Frolida kwenye kituo cha kufanayia mazoezi wiki ya kwanza ya mwezi Julai.
Mazoezi yawachezaji tayari yalikwisha anza walimu na makocha wameruhusiwa kuongoza mazoezi ya mtu na mtu.


Latifa juma mohamed
Habar mbaya, mungu amsaidie
Theckla
Pole yake jamani
Aziza mushi
Habari mbaya hizi jamn pole yake.
Mwanahamisi
Pole yake
Dorophina
Habari mbaya pole yake atakaa sawa tu
Magdalena
Sad news Yan huu ugonjwa hatari Sana Mungu tu atutetee pole Sana kwake
Zeiyana
Duuh..!pole sana Malcolm
Tatu
Du ili gonjwa hatari
Caroline
Atapona inshallah
Lydia Emmanuel Magoti
Duu pole yakee konjwa tishio
Ester mmakasa
Daah! Inabidi ajifukize na miarobaini ili virusi viondoke na ajitenge haraka sana ili asiwaambikize wezake ,pole kwake.
Ernest
Kumbe Marekani hali bado tete sana!!!!
Tahiya
Get well soon sharobaro wa NBA corona ipo tuchukuwe taadhari
Sadick
Baadhi ya nchi maambukizi ni makubwa hata hivyo tunapaswa kujipanga namna ya kuishi nao na mambo mengine yaendelee#meridianbettz
JULIANA
Jamani pole yake,huu ugonjwa bado upo aise
Gabriel
Ni habar ya kusikitisha sana kwa pacers Malcolm Brogdon kukutwa na maambikiz ya virus vya korona na pia mashabiki wa basketball tunayofuraha kupata matuman yabkurejea kwa lig ya NBA julai
Sad news 😢 & Good news 👍
#meridianbettz
Antony Luseno
Hii janga bado lipo japo kwa sasa kama limewekwa pembeni
Asia Abdy
Duh pole yake
Furahav
Hii civid 19 itawamaliza wamalekani.
Ester jackson
Pole sana kijana
Frank Patrick
Get well soon
Sabrina
Maoni:Daaah pole sana bhana
Omary lukumbi
Duuuh ina bidi awekwe karantin kusubir mpk hali yake ikae sawa ndio aweze kujumuika na wenzie janga noma sana
David Pere
Kweli huu ugonjwa hautaisha mapema maana bado inasumbua watu tu
Evaluziga
Jaman iligonjwa bado lipo tujiazali tunajiachia tu Aya pole yake mungu atamsaidia atapona
Povel
Get well soon 😘