Malcolm Brogdon Akutwa na Virusi Vya Korona.

Mchezaji wa kikapu kutoka timu ya Indiana Pacers Malcolm Brogdon amethibitishwa  kupimwa na kukutwa na Virusi vya Korona.

Brodgon mwenye umri wa miaka 27 amekuwa akionesha jitihada za kupigania haki za usawa kwenye jamii tangu kuzuka kwa janga la Korona mwezi machi hivyo kupelekea shughuli nyingi kusimama.

Msimu wa NBA 2019-20 unatarajia kurudi katika viwanja vya Disney World katika mji wa orlando mwashoni mwa mwezi  julai, na wachezaji wameripotiwa kuanza kujinoa kwenye vituo vyao wiki hii.

“Hivi karibuni nilipima na nimepatikana na maambukizi ya Virusi vya Korona kwa sasa nipo karantini,” Brogdon alisema.

“Naendelea vizuri, na ninatarajia kujiunga na wachezaji wenzangu mwishoni mwa mwezi julai kwaajili ya kuendelea na msimu wa NBA kwa michezo ya awali.”

Brogdon alijiunga na Indiana Pacers akitokea Milwaukee Bucks mwaka 2019 na huu ndio msimu wake wa kwanza akiwa na Indiana Pacers. Pia Brogdon alikuwa nje ya kikosi kutokana na majeraha kabla ya ligi kusimama mwezi machi, lakini mwezi Aprili ilielezwa kuwa yupo sawa kiafya kwa “100%.”

Pacers wamepanga kutua Frolida kwenye kituo cha kufanayia mazoezi wiki ya kwanza ya mwezi Julai.

Mazoezi yawachezaji tayari yalikwisha anza walimu na makocha wameruhusiwa kuongoza mazoezi ya mtu na mtu.

26 Komentara

    Habar mbaya, mungu amsaidie

    Jibu

    Pole yake jamani

    Jibu

    Habari mbaya hizi jamn pole yake.

    Jibu

    Pole yake

    Jibu

    Habari mbaya pole yake atakaa sawa tu

    Jibu

    Sad news Yan huu ugonjwa hatari Sana Mungu tu atutetee pole Sana kwake

    Jibu

    Duuh..!pole sana Malcolm

    Jibu

    Du ili gonjwa hatari

    Jibu

    Atapona inshallah

    Jibu

    Duu pole yakee konjwa tishio

    Jibu

    Daah! Inabidi ajifukize na miarobaini ili virusi viondoke na ajitenge haraka sana ili asiwaambikize wezake ,pole kwake.

    Jibu

    Kumbe Marekani hali bado tete sana!!!!

    Jibu

    Get well soon sharobaro wa NBA corona ipo tuchukuwe taadhari

    Jibu

    Baadhi ya nchi maambukizi ni makubwa hata hivyo tunapaswa kujipanga namna ya kuishi nao na mambo mengine yaendelee#meridianbettz

    Jibu

    Jamani pole yake,huu ugonjwa bado upo aise

    Jibu

    Ni habar ya kusikitisha sana kwa pacers Malcolm Brogdon kukutwa na maambikiz ya virus vya korona na pia mashabiki wa basketball tunayofuraha kupata matuman yabkurejea kwa lig ya NBA julai
    Sad news 😢 & Good news 👍
    #meridianbettz

    Jibu

    Hii janga bado lipo japo kwa sasa kama limewekwa pembeni

    Jibu

    Duh pole yake

    Jibu

    Hii civid 19 itawamaliza wamalekani.

    Jibu

    Pole sana kijana

    Jibu

    Get well soon

    Jibu

    Maoni:Daaah pole sana bhana

    Jibu

    Duuuh ina bidi awekwe karantin kusubir mpk hali yake ikae sawa ndio aweze kujumuika na wenzie janga noma sana

    Jibu

    Kweli huu ugonjwa hautaisha mapema maana bado inasumbua watu tu

    Jibu

    Jaman iligonjwa bado lipo tujiazali tunajiachia tu Aya pole yake mungu atamsaidia atapona

    Jibu

    Get well soon 😘

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.