Inaendelea..
Lazima ndani ya Barcelona kuna umoja, ukaribu na urafiki. Lakini aina ya mashabiki ambao Suarez atawakumbuka na mazoea kama mwanadamu wa kawaida, hivyo ni lazima kumwaga chozi. Yote sawa, lakini kama utabahatika kusoma kitabu chake hicho utagundua mapenzi yake na Barcelona hayakuanza wakati anakwenda kujiunga nayo lakini Barcelona imo ndani ya maisha yake kupitia Sofi.
Suarez hakupenda shule, ukizingatia familia yake ilikuwa ni ya kimasikini sana, hawakuwa na muda wa kuifuatilia sana mienendo yake shuleni. Lakini Sofi alipinga mara zote na kumhimiza kusoma. Muda mwingi, Suarez alilazimika kuazima nauli asafiri zaidi ya kilomita 30 kwenda kumtembelea Sofi nyumbani kwao. Baadaye familia ya Sofi ilihamia Ulaya, ilihamia jijini Barcelona mwaka 2003 na huu ndio ulikuwa mwanzo wa Suarez kutamani kwenda kucheza barani Ulaya kwa kuwa alitaka tena kuungana na Sofi ambaye alimuona ndiye tegemeo katika kila kitu kwake. Mara moja, alialikwa Ulaya na Sofi na bado anavyokumbuka walivyoibia kwenda kupiga picha ndani ya Uwanja wa Camp Nou kwa kuwa hawakuwa na fedha za kulipia zoezi la kutembelea uwanja huo. Unaona namna maisha yalivyokuwa na baada ya kurejea Uruguay, aliamua kufanya juhudi kuu, akapambana hadi alipofanikiwa kusajiliwa na klabu ndogo ya Groningen ya nchini Uholanzi, hii ilikuwa ni mwaka 2006.

Suarez aliongeza juhudi akijua alistahili maisha bora kwa kuwa Ulaya ni mapambano zaidi na mara nyingi alitaka kumridhisha Sofi kwa kuwa alijua alivyompigania na yeye hakuwa na elimu wala hakuwahi kufaulu, hivyo alipambana akijua mkombozi ni mpira. Alifanikiwa kujiunga na Ajax mwaka 2007, mwaka 2011 akatua Liverpool na 2014 ikawa ni Barcelona lakini kumbuka mwaka 2013 alitaka kujiunga na Arsenal lakini Steven Gerrard wakati huo akiwa nahodha wa Liverpool, alimzuia na kumueleza acheze msimu mmoja akiwa Anfield na huenda akajiunga na Real Madrid, Bayern Munich au FC Barcelona na si Arsenal tena, na kweli msimu uliofuata, hilo likatokea.
Unaona kiasi gani Mji wa Barcelona ulivyokuwa sehemu ya kumvuta Suarez kwenda Ulaya, kwa kuwa ulikuwa mji wake wa kwanza kukanyaga akiwa Ulaya lakini mapenzi yake na Barcelona, yalimfanya asichoke sababu alitamani siku moja ataichezea. Bila shaka ilikuwa ni klabu yake pendwa ambayo alifanikiwa kuifikia. Sofi, anabaki kuwa shujaa wake kwa kuwa unaona alivyoshiriki katika maisha yake wakiwa watoto kutoka katika familia zenye aina tofauti kabisa. Kwani baba mzazi wa Sofi alikuwa bosi wa benki na walihama baada ya benki kufungwa kutokana na anguko la kiuchumi mwanzoni mwa miaka ya 2000.
Chozi la Suarez si kuondoka tu FC Barcelona, linajumuisha mengi na “undugu” wa historia ya maisha yake na Jiji la Barcelona, unamfanya akumbuke mengi aliyopitia akijua sasa anahamia katika jiji pinzani la jiji lake kipenzi, timu yake kipenzi lakini maisha, hayakupi nafasi ya kuchagua kila unachokitaka kama leo Suarez ni tajiri, maisha yake ni ya kifahari kwa kuwa mshahara wake kwa mwaka utakuwa zaidi ya pauni milioni 6 (zaidi ya Sh bilioni 17), lakini hana ujanja, lazima aondoke Barcelona kwa maana ya klabu na jiji pia.
Beti kwa Kitochi Kushinda 300,000,000!
Unajua kuwa unaweza kushinda milioni mia tatu kwa buku tu? Ndiyo! Unaweza kushinda kwa kupiga *149*10# na kubashiri. Ingia mchezoni!


Issa
Suarez alikua mtu muhim barca sema kocha hakuwa na mahesabu nae lakin ni fowad makin na hilo amelionyesha mechi ya kwanza atletico kwa kupiga goli 2
Sabrina
Duh kumbe Suarez aliipenda barca kwa sababu ya historia yake na jiji la Barcelona pamoja na kumfata sofi nashukuru kwa kunijuza
Shani
Suarez ni mchezaji makini sana barca imepoteza kumuacha huyu
Amiri Kayera
Striker Bola kuwah kutokea alikiwasha San alivokua Liverpool
Rehema
Asante kwa taarifa
felister
dah barca wamemkatili sana Suarez
Samira
Kocha nazani hakumpenda tu Suarez ila ni mchezaji mzuri sana
magdalena
suarez apige moyo konde asonge mbele kocha wa barca alishamkataa kitambo tu
Elika
Dah Suarez piga moyo konde
Adelta
Suarez maisha popote angalia ndoto zako zitimiye
Dorophina
Suarez alikuwa na mapenzi ya dhati na timu yake alitamani kuitumikia mpaka mwisho
Angelina
Suarezi kikubwa maslahi tu popote kambi
Mwajumah
Barca awamefanya makosa sana kumuacha suarez kwan ni mchezaji mzuri sana
Fatina mfingi
Maisha popote kikubwa timiza ndot zako!
Caroline
Suarez ana mchango mkubwa sana Barcelona
Ester jackson
Baadae Barcelona watakuja kajuta kumpoteza
Tatu
Suarez akutaka kuondoka kabisa Barcelona sababu alikuwa na mapenzi nayo kutoka moyoni tatizo kocha akupendeza abakie pale
Lydia Emmanuel Magoti
Duu kweli Suarez Barcelona kwenye moyo wake inamchango mkubwa ndomana lazima angiwe nasimbazi Sana kundoka hapo kwenye krabu ya Barcelona ila mzeebaba usikate tamaa kokote kambi utapata ukitakacho Suarez piga kaz
Ernest
What a touching story!!! Suarez lives already on his dream now its a time to wish and dream for the new things
Neema
Kumbe aliipenda timu yake. Duu maisha popote usijal
Salma ngende
Dah! Hii aikuwa sahihi
aisha
Popote kambi cha msingi akaze tuu
Khadija
Kwani kambi popote
Nasra
Suarez kiboko
Saupha mohamed
Suarez yupo vizurii
Venerose
Suarez kikubwa maslai
David Pere
Suarez alikua mtu muhim barca sema kocha hakuwa na mahesabu nae lakin ni fowad makin na hilo amelionyesha mechi ya kwanza atletico kwa kupiga goli 2
Sauda
Barca wamemfanyia vibaya Suarez
Hopemwaikuka
Kila LA heri hata hapo
Povel
Suarez dunia mApito wanadamu soon watu wakuwah min ni vigeu geu sana
Gabriel
kocha hakuwa na mahesabu nae lakin ni fowad makin