Mourinho Afungiwa Mechi Moja na UEFA.

Bosi wa Tottenham Jose Mourinho amepokea adhabu ya kukosa mchezo mmoja katika mashindano ya Ulaya, UEFA imetangaza.

Mourinho amekutana na rungu hilo baada ya kuchelewa kufika katika mchezo wao waliyopoteza kwa 1-0 kwenye michuano ya Europa dhidi ya Royal Antwerp mwezi Oktoba 29.

Bosi huyo wa Spurs alipatikana na kosa na atawajibishwa baada kuchelewa kufika katika dimba la Bosuilstadion mjini Antwerp mwezi uliyopita, ingawa adhabu hiyo ilimsababisha awekwe kwenye matazamio ya kipindi cha mwaka mmoja, kuanzia tarehe ambayo maamuzi yamefanyika.

Tottenham pia ilipigwa faini ya €25,000 (£23,000) kwa kuchelewa kwenye mchezo huo wakati timu hiyo ya Premier League pia ilitozwa faini nyingine ya €3,000 (£2,600) kwa kukiuka sheria ya UEFA

Spurs wapo juu kwenye kundi J katika mashindano ya Europa baada ya mechi tatu mbele ya Antwerp na LASK ambao wana alama sawa lakini wemtofautiana magoli.

Timu ya Mourinho imepata ushindi wa pili katika michezo 10 ya Europa League baada ya kuifunga Ludogorets mapema mwezi huu.

Harry Kane amekuwa mchezaji wa tatu wa Tottenham kufunga 200 katika mashindano yote baada ya Jimmy Greaves (266) na Bobby Smith (208).


UMEJARIBU HII POKER YA VIDEO?

Jaribu sasa hapa Meridianbet. Ukiacha ukweli kuwa itakupa burudani maridadi, bado inakuhakikishia ushindi mkubwa. Kazi kwako kukusanya ushindi!

Meridianbet Casino

INGIA MCHEZONI!

22 Komentara

    Mourinho jifunze kwenda na muda

    Jibu

    Yani ni majanga

    Jibu

    Ndo ajifunze kutokana na makosa

    Jibu

    acha tu afungiwe ili siku nyingine ajifunze makosa yake

    Jibu

    Duu sio poa azabu kali hiyo

    Jibu

    Duuh atali na nusu

    Jibu

    Mourinho atajifunza kutokana na makosa

    Jibu

    Mourinho ndio atajifuza siku nyingine

    Jibu

    Kwa adhabu hii natumai atajifunza na kosa lake

    Jibu

    Pole sana Mourinho

    Jibu

    Mourinho tatzo anajikuta mjuag sana

    Jibu

    Mourinho ana maneno mengi muda wote anahis marefa wanamfanyia tofauti

    Jibu

    Sheria imefuata mkondo wake hapo

    Jibu

    Jose mourinho amekua anawashushia lawama marefa kwa kipind kirefu

    Jibu

    Duuh ila sheria ni msumeno

    Jibu

    Atajifunz jmb

    Jibu

    Kwa adhabu hii natumai atajifunza na kosa lake

    Jibu

    Pole sana

    Jibu

    Mourinho n mtukutu miaka yote,,kashafungiwa mara kibao akiwa italia hata Hispania.

    Jibu

    Mourinho sio poa ni mkorofi kidogo haya mambo lazima ya mtokee

    Jibu

    Duuh

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.