Lionel Messi ametoa mchango wake kwa Diego Maradona siku ya Jumapili wakati akishangilia goli jambo alilofanya kama “Surprise nzuri” kwa wachezaji wenzake wa Barcelona.

Mchezaji wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Maradona alifariki siku ya Jumatano akiwa na umri wa miaka 60 na alitolewa heshima kabla michezo yote ya LaLiga haijaanza wikendi hii.
Messi aliifungia timu yake goli la nne katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Osasuna na baada ya kufunga alivua tisheti yake ya Barca na kubaki na jezi ya Newell’s Old Boys klabu yake ya utotoni ambayo pia ni jezi aliyokuwa akivaa Maradona 1993-94.
Pia alionesha ishara ya saluti mawinguni kama heshima kwa mataifa mwenzake, ambaye alitumia msimu na klabu hiyo ya Newell’s ambako Messi alianza kucheza soka.
Antoine Griezmann na Philippe Coutinho wote walifunga katika ushindi mnono wa Barca pamoja na Martin Braithwaite ambaye alifunga goli la kwanza katika kipindi cha kwanza.
Walielezea kwamba walikuwa hawajui kitu ambacho Messi alikipanga siku ya leo katika dimba la Camp Nou ambako Maradona alicheza kutoka mwaka 1982-1984.
“Tumempoteza Maradona, kioo cha wachezaji wengi ulimwenguni tutamkumbuka sana,” Coutinho alisema.
“Hatukujua kama Messi amejiandaa kuonesha heshima kwa Maradona,” alisema Griezmann “Ilikuwa zawadi nzuri.”
Ushindi wa Barca unawasogeza mapa nafasi ya nane katika jedwali la LaLiga alama tisa nyuma ya viongozi wa ligi hiyo Real Sociedad.
Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.



Adelta
Inapendeza Sana kumuenzi rafiki yake
Lydia Emmanuel Magoti
Safiii lazima amuwaze alikuwa yuponae kalibu Maradona alikuwa nimtu wawatu Sana atakumbukwa daima maradona
Fatuma kasomo
Nimtazamo
Rahma
Nice
Dorophina
Maradona atakumbukwa daima Messi amefanya jambo la muhimu sana kumuenzi
Issa
Dunia imepoteza mtu
Hopemwaikuka
Utaish milele mioyon Mwa wapenz wa kabumbu
Sabrina
Pumzika kwa amani maradona
Magdalena
Messi kaonesha uungwana
Tatu
Bado sana watu kumsahau maradona
warda
Kumbe wametoka sehemu moja asante kwa kunijuza