Bondia nyota nchini Hassan Mwakinyo amesema kamwe hatishwi na rekodi za Brendon Denes wa Zimbabwe katika pambano la ubingwa wa Afrika wa ABU wa uzito wa Superwelter.
Mabondia hao watapanda uliongoni Mei 28 kwenye ukumbi wa Next Door Arena, na rekodi zikionyesha Denes HAJAPOTEZA hata pambano moja na ameshinda kwa KO katika mapambano MATANO kati ya nane aliyocheza.

Mwakinyo amesema kwa sasa anajiandaa vyema na pambano hilo na lengo lake ni kuendeleza ushindi ili kuendelea kutawala mchezo huo.
“Niko katika mfungo wa Ramadhan lakini sio kigezo cha kuacha mazoezi, bado naendelea tena kwa nguvu zaidi lengo langu ni moja tu kuwapa raha Watanzania kwa ushindi”.
Mbali na pambano hilo bondia Ibrahim Class naye atazichapa na bondia Sibusiso Zingangwe wa Afrika Kusini, wakati bondia nyota Shabani Jongo atapigana na bondia kutoka Nigeria, Olanrewaju Durodora.

TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO
Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!



Johnmary jo
Kujiamini ndo mpango mzima mwakinyo unaweza songa mbele#meridianbett#
Elika
Mwakinyo anajiamini sana
Mariam mtandama
Vizur
Adelta
Yuko vizuri
Shafii
Pambano litakua la aina yake ngoja tuone.
Khadija
Nice
Sarah
Yuko vizuri
Issa
Ngum jiwe
Sauda
Mwakinyo bingwa
Caroline
Mwakinyo oyee
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri
aisha
Jamaa anajikubali sana
neema hassan
Jamaa Yuko vzrii