TFF: Michuano Ya CAF 2021/2022 Kuanza Septemba 10

Shirikisho la soka Tanzania, TFF limetoa taarifa rasmi kutoka CAF kuhusu uhakika wa Tanzania kutoa timu nne zitakazoshiriki makombe ya Afrika, huku wakieleza kuwa taarifa rasmi kutoka CAF zinaeleza Tanzania itatoa timu nne.

Katika barua rasmi kutoka ukurasa wa Instagram wa TFF, shrikisho hili la soka lilieleza kuwa CAF wammeeleza kuwa Tanzania itakuwa miongoni mwa nchi zitakazotoa timu nne kushiriki michuano ya Afrika.

Kufanyika huko ni kutokana na ukweli kuwa Tanzania imejikusanyia alama nyingi kwa vilabu vyake vya Simba na Namungo kukusanya alama nyingi katika michuano ya klabu bingwa na shirikisho iliyopita!

Taarifa hiyo ya TFF pia ilieleza kuwa hatua ya awali ya michuano hiyo inatarajiwa kutimua vumbi rasmi mnamo mwezi wa tisa tarehe 10-12 huku zile za marudiano kupigwa mwezi huo huo tarehe 17-19.

Hatua ya makundi ya michuano hiyo inatarajiwa kuchezwa kuanzia Februari 11-13 mwaka 2022. TFF imeeleza kuwa Tanzania imekuwa nchi moja kati ya 12 zitakazotoa timu nne katika michuano hiyo mikubwa Afrika.


USHINDI BILA MIPAKA!

Hakuna mipaka ya ushindi kwenye Keno Instant ya meridianbet Kasino, hii wewe ndiyo una uamuzi zaidi juu ya mchezo na nafasi ya machaguo kibao
Arsenal, Arsenal Wawasilisha Ofa ya Pili Joaquin Correa., Meridianbet

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.