Dunia ina Paul Pogba wawili, Siku Paul Pogba wa Manchester United atakapoamua kumuiga yule Paul Pogba wa Ufaransa, Manchester United itatwaa ubingwa epl, UEFA na klabu bingwa ya dunia, halafu sisi mashabiki wa timu zingine tutakosa pa kupita.
Kama kuna mtu mshale wake wa saa unarudi nyuma kwa kasi, kabla hata ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo basi ni Karim Benzema. Hata Noel La Graet atakuwa anamtazama kwa aibu akikumbuka kwamba alimbania nafasi ya kwenda kombe la dunia kwa hivi vitu anavofanya.

Kwa sasa Ole Gunner Solksjaer atakuwa anajitazama akimuuliza Mungu ni kosa gani kubwa alilifanya mpaka ampitishe katika nyakati ngumu kama hizi. Wakati akisikitika kumcheza Victor Lindelof nafasi ya Harry Maguire, ghafla anamuona Raphael Varane juu ya machela akienda nje baada ya dakika 40 kwasababu ya majeraha.
Mtu mwingine anayeona asubuhi haifiki kabla hata ya walinzi ni yule mzee muhuni Fiorentino Perez. Miwani yake itakuwa inatazama kalenda yake na kuiuliza kwanini siku hazisogei akikumbuka kwamba yule Kylian Mbappe mkataba wake unafika mwisho na yupo tayari kujiunga na Real Madrid bure kabisa. Kwa Perez kumpata yule mtoto bure, ni sawa na kuokota paundi milioni 200 nje ya ofisi yake.
Yule Sergio Busquets, inabidi uwe na elimu walau level ya ‘PHD’ kuzielewa pasi zake. Hata Pep Guardiola atakuwa anatamani wale watoto wake wawili, Rodrygo na Gundogan wawe na akili yake, wacheze mpira kama wake pale nyumbani kwake.

Kazi nyingine ngumu duniani tukiachana na kubadili fikra za msichana aliyependa, ni mwamuzi kutafsiri sheria za soka uwanjani kwa haki na kila mtu kuridhika. Lile bao la pili la Mbappe lingeweza kuamuliwa offside na kila mtu akaridhika. Nazidi kupata mashaka kwamba hata malaika wakishushwa wacheze mechi bado watalaumiwa tu.
Fanya wiki yako iwe ya kuvutia zaidi, tunaelekea Los Angeles kutengeneza mkwanja na kasino maridhawa ya LA Rouge kutoka katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Fursa ya kufurahi huku unajaza pochi yako.

CHEZA HAPA

