Baada ya kuruhusiwa[Jonathan Irons] kutoka gerezani, mwanadada Maya Moore alijikuta akipiga magoti kwa furaha.
Baada ya kupambana bila kuchoka, hatimaye Moore amemwona na kumshukuru Irons baada ya miaka 23. Amenukuliwa akisema , ” Sawa, yametimia”

Ifahamu safari ya Moore na Jonathan Irons.
Mapema Julai 28, msimu mpya (2020) wa WNBA ulianza rasmi. Safari hii, The Minnosota Lynx watakuwa wanalenga kubeba ubingwa kwa mara ya 5. Japokuwa, kwa mara ya kwanza msimu huu Lynx watawakosa baadhi ya wachezaji wao nyota.
Mwaka 2011, Moore alikuwa mchezaji wa kwanza kuchaguliwa Lynx. Aliwasaidia kubeba kombe la Championship mara 4 na mwaka 2014 alitajwa kama MVP. Akiwa na umri wa miaka 31, Moore anamedali 4 za dhahabu – 2 za Olympic na 2 za World Champions.
Mwaka 2019 aliushangaza ulimwengu kwa kuamua kuzitoa medali zake zote kwa ajili ya mwanaume aliyekutana nae miaka 12 iliyopita. Mwanaume ambaye amekuwa kama kaka kwake.

Mwaka 1997 [Jonathan Irons akiwa na miaka 16] kunashambulizi lilifanyika St. Louis, Missouri ambapo mtu mmoja alivamia nyumba ya Stotler na baada ya Stotler kurejea, mtu yule alimshambulia kwa risasi.
Japokuwa Stotler hakupoteza maisha, alipaswa kutambua aliemfanyia tukio lile katika picha za washukiwa wa shambulizi lile. Mwanzoni alishindwa kumtambua mhusika lakini ofisa wa polisi walimtaka ajitahidi kwa uwezo wake wote kutambua picha ya mtu anaemjia kwenye kumbukumbu zake, aliichagua picha ya Jonathan Irons. Lakini hakukuwa na uthibitisho wowote wa DNA au damu unaochagiza uhusika wa Irons.
Mtetezi wa kijamii hakuruhusu Irons kusimamishwa kizimbani kwa dai la kwamba ni mtoto mdogo, hakuhusika na hakuwa na elimu. Upande wa mashtaka ulikiri Irons kuhusika kitu ambacho yeye[Irons] pamoja na mawakili wake walikanusha.
Mshataki alisema ” usimtetee kwa sababu ni mdogo. Ni mtu hatari kama mtu aliyemzidi miaka 5. Tunatakiwa kufundisha hawa vijana kwamba, kama utafanya vitu kwa kikubwa na wewe utahukumiwa kama mtu mkubwa.”
Mwaka 1998, Irons alihukumiwa kwenda jela kwa miaka 50. Mwaka (2007) Moore akiwa na miaka 18 alisafiri kwenda Missouri kusalimia familia yake na ndipo alipokutana na Irons. Baada ya hapo alikuwa akienda kumsalimia mara kwa mara na kumtumia vitabu alivyokuwa anavipenda.
Katika hali ya kushutukiza aliamua kupumzika kucheza mchezo wa vikapu kwasababu aliamini Irons alikuwa anasema ukweli. Moore alinukuliwa akisema, “kunakitu katika ukweli ambacho kinakufanya uone kitu fulani kinatokea. Alipaswa kuendelea kuamini hivyo na kama tutausema ukweli kwa mtu anayestahili kuusikia, basi mtu huyo atafanya maamuzi sahihi.”

Mapema mwaka 2019 wakati ambapo alitakiwa kujiandaa na msimu wa WNBA, Moore aliamua kuutumia muda wake kufanyia kazi suala la Irons akishirikiana na wanasheria na wakaomba kesi yao kurudia kusikilizwa.
Baada ya miaka 21, bado upande wa mashtaka wa serikali haukutaka kushindwa na walijitahidi kupingwa kesi kurudiwa. Jitihada zao ziligonga mwamba na Oktoba 2019, Irons alipewa nafasi ya kusikilizwa mbele ya mahakama.
Mwezi Machi 2020, kesi ya Irons iliamuliwa. Jaji Daniel Green alitaja maamuzi yaliyofanyika awali kuwa ni ‘dhaifu’. Kwa mamlaka yake, jaji alisema alama za vidole zilizopatikana kwenye mlango wa Stotler, hazikufanana na za Stotler wala Irons. Hii ilithibitisha kwamba muhusika alikuwa ni mtu mwingine na sio Irons.
Hii inaonesha kwamba, kuna muda ili mabadiliko yatokee, takwimu pekee hazitoshi. Panahitajika stori ya kweli ya mtu fulani.
Drops and Wins!
Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.


Dorophina
Moore yupo vizuri sana kwenye kikapu
Nasra
Gud news
Lydia Emmanuel Magoti
Makara nzuri nime hilewa hii
aisha
Ahsante kwa habari
Ester jackson
Daah inahuzunisha sana pia pongezi kwa ushindi wa kuwa huru tena
rama
Maoni:th
Fatina mfingi
Asanteh kwa taarifa meridianbet
Latifa juma mohamed
Moore ni mchezaji mzur Sana wa WNBA ,it’s sad story.
rama
Maoni:thank u kwa update
Povel
Thnks kwa update za michezo na burudani
Furahav
Habari nzuri.
Devotha
Moore yupo good sana
Gabriel
Japo Moore ni mchezaji mzur kwny lig ya WNBA pia n mchezaji mwenye mafanikio makubwa sana
Sabrina
Hongera jonathan Irons kwa kuwa huru
farida ahmadi
Pongezi Sana Moore
Shan
Moore Big up!
Magdalena
moore yupo vizuri sana anajituma katika kikapu #meridianbet
Tatu
Hongera zake
felister
Moore yupo vizuri
Samiah
Yupo vzr Moore
warda
Yupo vizuri sana
Ernest
Moore amefanya jambo la kishujaa sana dhidi ya Irons