Nyota wa Barcelona anayechipukia Ansu Fati ameitwa katika kikosi cha Hispania kwa mchezo dhidi ya Ujerumani mwezi ujao.
Winga wa Wolves Adama Traore ni mchezaji mwingine aliyeitwa katika kikosi hicho, alishindwa kucheza mchezo wake wa kwanza wa kimataifa mwezi Novemba mwaka jana kutokana majeraha.
Katika hali ya kukiweka sawa kikosi, kocha mkuu Luis Enrique pia alimuongeza mlinzi wa Manchester City Eric Garcia na kiungo wa Real Madrid Oscar Rodriguez, ambaye alikuwa Leganes kwa mkopo.
Pia kuna nafasi chache kwa wachezaji Ferran Torres,Golikipa wa Athletic Bilbao Unai Simon, kiungo wa Real Sociedad Mikel Merino na beki wa Madrid Sergio Reuilon.
Beki wa kushoto wa Barcelona Jordi Alba ameechwa pia hakuna mchezaji yoyote wa Atletico Madrid kwenye kikosi hicho.
Mchezo wa Septemba utakuwa mchezo wa kwanza tangu mwaka jana, kwa mchezo wa kimataifa wa mwezi Machi ulihairishwa kufuatia kuwepo kwa janga la virusi vya Corona.
Wanaelekea kukabiliana na Ujerumani mwezi Septemba 3 kabla ya kuwaongoza Ukraine siku tatu baadaye.
Kikosi kizima cha Spain: David de Gea (Manchester United), Kepa Arrizabalaga (Chelsea), Unai Simon (Athletic Bilbao); Jesus Navas (Sevilla), Dani Carvajal (Real Madrid), Sergio Ramos (Real Madrid), Pau Torres (Villarreal), Diego Llorente (Real Sociedad), Jose Gaya (Valencia), Sergio Reguilon (Sevilla), Eric Garcia (Manchester City); Fabian Ruiz (Napoli), Thiago Alcantara (Bayern Munich), Sergio Busquets (Barcelona), Rodri (Manchester City), Mikel Merino (Real Sociedad), Dani Olmo (RB Leipzig), Oscar Rodriguez (Leganes); Rodrigo Moreno (Valencia), Mikel Oyarzabal (Real Sociedad), Adama Traore (Wolves), Marco Asensio (Real Madrid), Ansu Fati (Barcelona), Ferran Torres (Manchester City).
Drops and Wins!
Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.


aisha
Pole sana Ansu kwa majeraha uliyokua umepata lakini mungu anesaidia
rama
Maoni:safiii hispain ya vijana sasa
Nasra
Majeraha yatapona tu
Ernest
Mwanzo mzuri kwa Ansu Fati
Saupha mohamed
Pole sana
Ester jackson
Habari njema sana
Povel
Gud STart for Ansu Fati and Adam Traore natumain wataonesha kitu kwny national timu
Zeiyana
Niwakati wake ansu fati kuonesha kiwango chake
Lydia Emmanuel Magoti
Habari nzuri kwake kwakurudi kwenye kikosi kivingine dogo
Adelta
Habari njema kwa ansu Fati@meridianbettz
Magdalena
mambo mazuri yaja spain
Gabriel
Kikosi kiko vzur sana nimekipenda
Mwajumah
Habari njema sana#Meridianbettz
Adelta
Habari njema kwa ansu fati
Furahav
Hongera zao.
Sylvester
Kitakua kikosi bora sana ila nilikua sijui kama Adama Traore ni Mspain,Asante kwa taarifa
Mwanahamisi
Pole sana
Salma ngende
Kikosi kipo vizuri
Sabrina
Nawatakia kila la kheri Ansu Fati na Adam Traore wafanye vizuri katika timu yao ya taifa dhidi ya ujerumani mwezi ujao
Dorophina
Kila lakheri ansu fati katika safari yenu ya mpira klabu nyingine
Khadija
Habari njema
Amiri Kayera
Habar nzur
Fatina mfingi
Mambo Ni Moto!!
Sadick
Hbari njema kwa chipukizi wanajituma zaidi kucheza timu za taifa#meridianbettz
Devotha
Habari njema
farida ahmadi
Habari njema Sana
Theonestina
Pole yake
Janeflora malisa
Nice
Latifa juma mohamed
Nice information.
David Pere
Kitakua kikosi bora sana ila nilikua sijui kama Adama Traore ni Mspain,Asante kwa taarifa
Fatuma kasomo
Kikosi kipo vizuri sn
Shan
Habar njema kwa wanao chipukia kwenye game!!
warda
Wawooo iko poa sana
Mwajumah
Mwanzo mzuri kwa Ansufati#Meridianbettz
felister
hicho kikosi kitakua bonge moja la kikosi yaani ni balaa
Tatu
Ansu fati ni mchezaji kwenye kipaji kikubwa
Samiah
Pole yake
Hope mwaikuka
ANSu 💪💪
marry
pole kwake
Issa
Safi ansu kuitwa kikosin
Shafii
Habari nzuri kwake ni wakati wa yeye kuonesha uwezo wake.