Pitso Mosimane kocha wa zamani wa klabu ya Al Ahly ya nchini Misri pamoja na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini amejiunga na klabu ya Al-Ahli ya nchini Saudia Arabia.

Kocha huyo mwenye mafaniko makubwa katika soka la Afrika ametangazwa na klabu hiyo mapema leo hii ni baada ya kuachana na klabu ya Al-ahly miezi kadhaa iliyopita.

pitso mosimaneMosimane anajiunga na klabu ya Ahli inayoshiriki ligi kuu nchini Saudia Arabia baada ya kufanya makubwa katika soka la Afrika kwa kubeba Kombe la mabingwa Afrika kwa ngazi ya vilabu mara tatu.Akibeba mawili na klabu ya Al-Ahly ya nchini Misri na moja akiwa klabu yake ya nyumbani Afrika ya Kusini Mamelodi Sundowns pamoja na makombe ya ndani ya ligi zote alizocheza nchini Misri akiwa bingwa mara moja huku Sundowns akibeba mara tano.

Mosimane anabaki kua kocha aliefanya vizuri zaidi katika soka la Afrika katika miaka ya karibuni licha ya kuondoka ndani ya hili lakini anabaki kama alama ya soka la Afrika kwa upande wa makocha.


 


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa