UONGOZI wa klabu ya Pan African imemalizana na mfungaji wa bao pekee la Mbao kwenye mchezo wa Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Singida Big Stars, Nasri Daudi kwa mkataba wa mwaka mmoja. 

Nasri ambaye anacheza eneo la kiungo mshambuliaji tayari ameanza mazoezi na kikosi hicho ambacho kitashiriki michuano ya Championship kwa msimu huu.

Pan, Pan Yamalizana na Muuwaji wa Singida Big Stars , Meridianbet

Akizungumzia usajili huo, Ofisa Habari wa Pan African, Leen Essau amesema kuwa: “Tunayo furaha kubwa kumtambulisha rasmi kiungo mshambuliaji, Nasri Daudi akitokea Mbaofc kwa mkataba wa mwaka mmoja.

“Ongezeko la nyota huyu kwenye kikosi chetu kitaenda kutusaidia kwenye eneo la mbele kutokana na mapungufu ambayo tuliyaona kwa msimu uliopita.

“Kikosi tayari kimeanza maandalizi ya msimu ujao na tayari tumecheza mechi nne za kirafiki ambazo ni za ndani katika kuhakikisha muunganiko I napatikana kwenye timu.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa