Harry Kane Hapoi Haboi!!

Unakumbuka Harry Kane alipoanza kufunga na kudhaniwa atakuwa mchezaji wa msimu mmoja tu? Haikuwa hivo, tangu alipoanza kutisha kwenye msimu wake wa kwanza, hajawahi kuporomoka uwezo tena. Wala haoneshi dalili za kuporomoka.

Mabao yake mawili aliyoyafunga kwenye ushindi wa 3-1 kwa Tottenham dhidi ya Newcastle, hayakumfanya tu kufikisha mabao 20 kwa misimu wa sita mfululizo bali alifungua ukurasa mpya wa mabao 200. Kati ya hayo, 185 ameyafunga akiwa na uzi wa Tottenham, kisha mengine aliyafunga alipoenda kwa mkopo Millwall-9, Leyton Orient-5 na Leicester city-2

Katika hali ya kushangaza, imemchukua michezo 350 tu kufikisha idadi hiyo ya mabao. Cristiano Ronaldo anayedaiwa kuwa moja kati ya wafungaji hatari kuwahi kutokea kwenye historia mpira wa miguu, ilimchukua michezo 29 zaidi ya Harry Kane kufikisha idadi hiyo ya mabao 200.

Si Ronaldo pekee, bali Harry Kane amefikisha mabao 200 kwa haraka zaidi kuliko Thierry Henry na Sergio Aguero. Wayne Rooney ambaye ni mfungaji wa pili bora wa muda wote wa epl, ilimchukua michezo 100 zaidi ya Kane kufikisha mabao 200.

Mourinho aliyefanya kazi na wachezaji wakubwa duniani alikuwa mmoja kati ya watu walioshangazwa na rekodi ya Harry Kane. Mourinho alisema  “inashangaza sana kumuona amefikisha mabao 200 akiwa na umri mdogo namna hii. Sitashangaa kumuona akiwa na mabao 200 mengine.”

Wayne Rooney amefunga jumla ya mabao 208 ya premier league, Harry ameshafunga 138. Je Kane ataweza kuifikia na kuivunja rekodi hiyo.


42 Komentara

    Harry kane yuko vizuri Sana kihalisia anajua majukum yake awapo uwanjani

    Jibu

    Kane ni mchezaji mzuri Sana hanajua hanachokifanya

    Jibu

    Uwezo anao mkubwa sanaa kwahiyo Moto wake unazidi kuwa mkali sanaa

    Jibu

    kanifanyia kazi nzur sasa degea azingue tena fala yule kama alivowapa chelsea ushindi bwege yule

    Jibu

    Harry kane ni mmoja kati ya watu wanaojielewa sana

    Jibu

    Kwa kiwango chake alicho onesha akiwa na juudi toka yupo na mri mdogo hataweza tu kufikisha hayo magoli ni yeye tu kujiamini na kuongeza juudi

    Jibu

    Kani Yuko vizuri kwenye uchezaji

    Jibu

    Kane yupo vizuri sana binafsi mimi namuelewa mno

    Jibu

    Anajitahidi sana#Meridianbettz

    Jibu

    Kani ni mchezaji mzuri sana#Meridianbettz

    Jibu

    Kane anajua mpira na anajua n Nini anafanya akiwa uwanjani

    Jibu

    Herry kane yupo vzr sana kwan anajua anachokifanya#meridianbettz

    Jibu

    Harry Kane kijana mahiri mwenye kasi yampira akiwa uwanjani tunaona anavyo jituma sana na anajua anacho kifanya yuko yofauti na wachezaji wezake wa Tottenham

    Jibu

    Hawezi kupoa ikiwa uwezo anao ,ni mchezaji wa kuigwa ,na anakipaji kikubwa sana

    Jibu

    Kane moto wake unazidii kuwaka kwa kweli asibweteke lakini

    Jibu

    Isingekuwa majeraha yanayomwandama kila baada ya muda kuvunja rekodi ya Rooney ni swala jepesi kwake

    Jibu

    anajua nini anachofanya anapokua uwanjani

    Jibu

    Herry Kane yupo vizuri sana nimchezaji anahejielewa anajituma kwenye kazi yake yupo vizuri kwamjula jembe uyo

    Jibu

    Kane hatari sana uwezo wake kwenye boksi ni moto sema majeraha yanamfanya awe nje mara kwa mara

    Jibu

    jamaa yuko vizuri alipeperusha sana bendera ya England

    Jibu

    Jerry Kane ni kijana anayejituma jitihada zake zinaweza kumfikisha mbali sana hapoi wala haboi

    Jibu

    Ni mchezaji mzuri anajituma sana ndo maana anafanya vizuri

    Jibu

    yani Harry Kane ni mchezaji mzuri na bora sana siku zote

    Jibu

    Binafsi naamini uwezo wa Harry Kane na kumtambua kama mchezaji hatari zaidi kwenye kufumania nyavu, Kwa msimu huu majeruhi yamemnyima raha na kumfanya kusuasua kwenye mbio za mfungaji bora

    Jibu

    Imekaa poa sana 👍

    Jibu

    Harry Kane ana njaa ya kufunga magoli naamini atafikisha magoli 500 muda mfupi kabla ya kufikisha miaka 30#meridianbettz

    Jibu

    Ni mchezaji mzuri

    Jibu

    Harry kane inabidi akacheze man u kutokana na uwezo wao.

    Jibu

    Namuelewa sana kane

    Jibu

    Kane yupo vzr sana

    Jibu

    Kane yupo vizuri sana

    Jibu

    Kane anajua mpira

    Jibu

    Harry Kane ni wakati wake sasa wa kutimkia club zenye mafanikio makubwa na yeye hajiweke mahari pazuri na mafanikio makubwa.

    Jibu

    Imekaa vizur sana

    Jibu

    Nimfungaj mzur san

    Jibu

    Namkubal sana kane

    Jibu

    Kane majeruhi tu yasimzidi ila anauwezo hata wakuzidi hiyo ratio anauwezo mkubwa wa kucheka na nyavu

    Jibu

    Jamaa yuko vizuri uwajani

    Jibu

    Hary kane yuko on fire

    Jibu

    Harry Kane ni wakati wake wa kutimiza ndoto zake

    Jibu

    Harry Kane yuko vizuri sana anapokua uwanjani

    Jibu

    Kweli kabisa

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.