Shirikisho la soka la Ujerumani halijawakuta na hatia klabu ya Bayern Munich kwenye sakata la kuchezesha wachezaji 12 hivyo madai ya kutaka mechi irudiwe yametupiliwa mbali na matokeo yata simama kama yalivyo.
Bayern iliinyuka Freiburg bao 4-1 mchezo wa Bundesliga wikendi iliyopita wakati pia kulitokea sintofahamu dakika za mwsiho baada ya Bayern kubainika kuchezesha wachezaji 12 hata hivyo hawataadhibiwa kwa kuwa kosa lilikuwa la waamuzi na siyo Bayern Munich.
Freiburg walipeleka malalamiko yao kwa DFB wakitaka kukata rufaa mchezo urudiwe sababu ya kubainika wachezaji wa Bayern kuzidi uwanjani kwa takribani sekunde 17 lakini juhudi zao zimegonga mwamba na matokeo hayata badilika.
Mwenyekiti wa DFB alisema: “Awali ya yote tchukulie kama wachezaji wote wa Bayern walikidhi kucheza.”
“Waamuzi hakutimiza kjukumu lao kujua idadi ya wachezaji uwanjani na mwisho wa siku waliendelea na mchezo bila kuangalia idadi ya wachezaji wanaoruhusiwa kucheza.
Ingawa mwamuzi Dingert alisema suala hilo lilitokana na makosa ya meneja wa timu ya Bayern, Kathleen Krüger, ambaye alionyesha namba isiyo sahihi ya mchezaji kwenye ubao wa kielektroniki. Wakati Süle alipoingia kwenye namba 29 namba ya zamani ya Kingsley Coman ilionyeshwa badala ya namba 11 namba ya sasa ya Coman, na kumwacha Mfaransa huyo bila kujua kwamba alipaswa kutoka.
Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.