Timo Werner anatarajia kuanza kupangwa kwenye kikosi cha The Blues baada ya kusajiliwa kwa dau la £45m akitokea klabu ya RB Leipzig msimu uliyopita.
Werner ni zao la akademi ya klabu ya Sturttgart, ana macho makali kama wembe katika goli.

alikuwa kinara wa upachikaji magoli katika kikosi cha U-19 akiwa na umri wa miaka 16 aliweza kutupia wavuni mabao 24 na kuona akitunukiwa medali ya dhahabu ya Fritz Walter- Pia alipata tuzo ya kifahari ya mwaka nchini Ujerumani.
Alifanikiwa kuwa mchezaji mdogo wa Stuttgart anayecheza katika kikosi cha wakubwa na kufunga mabao mengi mwaka 2013-14 kabla hajasepa na kutua RB Leipzig mwezi Julai mwaka 2016.
Akiwa chini ya mwalimu kijana Julian Nagelsmann, Werner alipeleka soka lake katika levo nyingine.
Akisakata katika eneo la mshambuliaji wa kati alionesha umahairi wake kwa kufunga mabao 78 na kutoa asisti 32 katika ligi ya Bundesliga kwenye misimu minne iliyopita.

Timo Werner akiwa na umri wa miaka 24,amefungua ukurusa mpya wa maisha yake ya soka nchini Uingereza katika klabu ya Chelsea na jinsi anavyo jiamini anaonekana kasi yake ya kutingisha nyavu za wapinzani itaendelea.
Katika mahojiano yake ya kwanza na klabu, alisema “tumeongea sana na kocha [Lampard] kuhusu mfumo na namna ninavyoweza kucheza vyema.
“Anataka kunisaidia sio tuu kama mchezaji bali kibindamu na kufikia malengo yangu najisikia vizuri sana nina furaha kuwa hapa.
“Mtindo wa mpira wa Premier League ni wa kasi sana na mimi napenda mtindo huo nina kasi sana nadhani ni sehemu sahihi mimi kucheza.
Ingawa haijafahamika ni mtindo gani Chelsea itautumia kwa msimu mpya lakini Werner anaonekana kuweza kuendana na mtindo wowote pale iatapo hitajika. Werner atashirikiana vyema na wachezaji kama Tammy Abraham au Olivier Giroud
Mabeki wa vilabu mbali mbali vya Premier League watakuwa na kazi kubwa ya kuweza kumzuia mtaalamu Werner pindi wakitua Stamford Bridge.
Ukweli Kuhusu Timo Werner
Umri: 24 Nafasi: Mshambuliaji
Utaifa: Ujerumani: (mechi 29, magoli 11) Klabu ya sasa: Chelsea Vilabu alivyovichezea: RB Leipzig (michezo 159, magoli 95), Stuttgart (mechi 103, magoli 14)
Beti Mbio za Mbwa Mubashara
Hii ni rahisi zaidi! Hapa USHINDI unaupata kwa kuchagua mbwa anayeshinda mbio na machaguo mengine yenye odds tamu.


Issa
Ni mchezaji mzuri sana toka akiwa rb amedhihirisha hilo lampard akimpatia walishaji wazuri basi hawatajutia usajili huu
Shafii
Record yake ni nzuri katika kupachika mabao atakua msaada mkubwa Sana darajani msimu ujao.
Povel
Mchezaj mzuri anarekodi nzuri ngoj tuone darajan ataonyesh kitu gan hapo thnks meridian kwa update
Genia Sikaluzwe
Ahsant meridian kwa taarifa
Sabrina
Hapo Sasa Chelsea ndio wamefanya usajili wamemleta mchezaji anaejielewa
Theonestina
Hongera Chelsea kwa kuleta jembe
Sadick
Ligi ya EPL ngumu, haijawahi kuwa rahisi kwa wachezaji kuzoea na kuwika tuone kama atawika Chelsea kama ilivyokuwa kwa Mjerumani mwenzie Michael Ballack#meridianbettz
Hope mwaikuka
Aisee wametishaa
Gabriel
Chelsea msimu naonwako vzur sana kweny usajil
Amiri Kayera
Ni kwer mchezaj mzur atawasaidia
marry
asante kwa update
Furahav
Yuko vizuri sana.
Samira
Anarekodi nzuri sana katika soka Chelsea wakimpata itakua poa sana
Latifa juma mohamed
Ana rekodi nzuri hakika huyu ni mwamba km jina lake linasadifu, Chelsea kikosi chaxid kuimarik.
Frank P
Akaribie epl
farida ahmadi
Yuko vizuri Sana
David Pere
Record yake ni nzuri katika kupachika mabao atakua msaada mkubwa Sana darajani msimu ujao.
Rehema
Big up Chelsea
rama
Maoni:karibu Chelsea
Sauda
Wametisha sana
Zeiyana
Wanajitaidi sana Chelsea kwa usajili huu hinawapa hamasa mashabiki wao..!
Tatu
Kijana ana history mzuri kwenye michezo
aisha
Chelsea mko vizuri kwa usajili wenu
Adelta
Chelsea wako vizuri kwenye usajili
@meridianbettz
magdalena
chelsea ni wakati wao sasa kusahihisha walipokosea na kujipanga upya
Caroline
Timo Werner ni mchezaji mzuri
Nasra
Yuko vzuri Sana
Ester jackson
Msimu huu Chelsea tuko vizuri sana tu nasubiri mchezo tu uwaze
felister
usajili konki wa chelsea
Ernest
EPL kuna changamoto Chelsea wasianze kutamba sana
Saupha mohamed
Good news
Lydia Emmanuel Magoti
Chelsea awamu itakayo kuja itakuwa Mambo mazuri mnasajili vifaa
Theckla
Wamelamba dume
Rose kapinga
Hatutaki sifaa tuuu,tunataka kuona maajabu yake!!!
jullie
safi sana
Dorophina
Habari njema kwa mashabiki wa chelsea
Asia Abdy
Nice
Samiah
Safi
Khadija
Hongera chelsea kwa kureta jembe#meridianbettz
Fatina mfingi
Hongeren Chelsea!!
Neema
Pongezi kwao Chelsea
warda
Hongera Yake Sana