Ramos Afunga Bao la Kwanza kwa PSG

Beki kisiki wa PSG Sergio Ramos alifunga goli la kwanza kwa timu hiyo tangu aliposajiliwa katika mchezo wa Ligue 1 siku ya Jumapili dhidi ya Reims.

Ramos Afunga Bao la Kwanza kwa PSG

Beki huyo alifunga goli katika kipindi cha pili katika uwanja wa Parc des Princes huku viongozi wa Ligue 1 wakifurahia ushindi mnono wa 4-0 dhidi ya Reims.

Ramos ilikuwa ni mechi yake ya pili kuanza ya ligi akiwa na PSG, akiwa na matatizo ya majeruhi kumaanisha kwamba amestahimili mwanzo mgumu wa maisha katika mji mkuu wa Ufaransa tangu alipohamia akitokea Real Madrid.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 alifurahi kurejea kwenye kikosi cha kwanza akifunga bao na kucheza dakika 90.

“Nina furaha sana kwa ushindi huu na kwa bao langu la kwanza na timu hii,” Ramos aliiambia Amazon Prime Video. “Nimefurahi nilicheza kwa dakika 90. Ninapenda kuungwa mkono na mashabiki. Ni vizuri kuchukua pointi tatu.

“Hili ni goli langu la kwanza na PSG na ninatumai kutakuwa na mengi zaidi. Jambo muhimu ni kuimarika kimwili siku baada ya siku na kuonyesha toleo langu bora kwa timu.”


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe