Timu ya Yanga ambao ni mabingwa wapya wa taji ya Ngao ya Jamii leo wameondoka na kuwafuata wapinzani wao kwenye Ligi Kuu Bara Kagera Sugar.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ilishinda taji la Ngao ya Jamii kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi.
Ilikuwa ni Jumamosi ya Septemba 25, Uwanja wa Mkapa ambapo bao la nyota mpya Fiston Mayele liliizamisha mashua ya Simba na kuwafanya waliyeyushe taji ambalo lilikuwa mikononi mwao.
Mchezo huo wa kwanza wa Yanga unatarajiwa kuchezwa Septemba 29 siku ya Jumatano, Uwanja wa Kaitaba.
Msimu uliopita kwenye mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Kaitaba, Yanga ilishinda bao 1-0 na kuondoka na alama tatu muhimu hivyo msimu huu wana kazi ya kulinda rekodi huku Kagera Sugar ikiwa na hesabu za kuharibu rekodi hiyo.
Ushindi walioupata unawafanya wawafuate wapinzani wao kwa kujiamini katika kusaka alama tatu muhimu.
Michezo ya ufunguzi leo itakuwa ni kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Mbeya Kwanza ambao wamepanda ligi kuu msimu huu pia mchezo mwingine utazikutanisha Coastsl Union dhidi ya Azam katika dimba la Mkwakwani
SPACE SPIN NA MERIDIANBET.
Ni Mabingwa pekee Meridianbet wanakupa nafasi ya kushinda zaidi na mchezo wa Space Spin katika kasino bomba za meridianbet. Ni wakati wa kufurahia na kutengeza mkwanja bila kuwaza.


