Kocha wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp hajakanisha tetesi za mchezaji wa zamnai wa klabu ya hiyo Steven Gerrard kuja kurithi mikoba yake ya kuinoa klabu hiyo miaka ya baadae.

Jurgen Klopp mwenye miaka 54, hivi karibuni amesaini mkataba mpya na klabu hiyo ambao utamuweka kwenye dimba la Anfield mpaka mwaka 2026, hii itamfanya kuwa kocha wa kwanza kuingoza klabu hiyo kwa miaka 10, tangu Tom Watson afanye hivyo mwaka 1900. Awali Klopp alisema kuwa ataachana na klabu hiyo baada ya muda wake kuisha.

Jurgen Klopp

Klopp alipoulizwa uwezekano wa Steven Gerrard kurithi mikoba yake kwenye dimba la Anfield alisema, “anaweza kuwa mrithi wangu? Ndio, bila shaka, inawezekana. Sina wazo lolote, sio maamuzi yangu ambayo nayafanya. Kwaiyo nadhani inawezekana, hivyo ndivyo ilivyo.”

Liverpool kwa sasa wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo nyuma ya Man City ambao wanaongoza ligi kwa alama tatu zaidi, na mchezo unaofuta ni Liverpool kuwafuata Aston Villa siku ya Jumanne kwenye dimba la Villa Park.

Jurgen Klopp kwenye kipindi chake tokea atue dimba la Anfield amefanikiwa kubeba ubingwa wa ligi kuu, ligi ya mabingwa ulaya na Carabao Cup. Huku akiwa na mchezo wa fainali ya FA Cup dhidi ya Chelsea na mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa na Real Madrid msimu huu.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa