Formula 1 imefuta mbio zilizopangwa kufanyika nchini Urusi za Russian Grand Prix leo siku ya ijumaa kutokana na nchi ya Urusi kuivamia Ukraine.
Chama kinachosimamia mashindano ya F1, FIA na timu shiriki siku ya alhamisi walifanya kikao kuhusu nafasi ya Urusi kwenye mchezo huo, kabla ya kufanya maamuzi hii leo ya kufuta mbio zilizopangwa kufanyika nchini urusi mwezi September.

Waraka uliotolea baada ya maamuzi ulisomeka, “tunatizama maendeleo ya ukraine kwa uchungu sana na mshutuko mkubwa na tunatumai mazungumzo ya haraka ya amani yatafanyika.”
Mashambulizi ya kijeshi yalioanza siku ya alhamisi, leo yameendelea tena kwa mara ya pili na jeshi la Urusi linakaribia kufika mji mkuu wa wa Ukraine Kyiv.
Meridianbettz na Aviator wanakupa mchongo wa kuibuka na iPhone 12 katika kasino ya Aviator itakayodumu kwa siku 7. Kuwa rubani wa Aviator na ujishindie!