Mshabuliaji wa timu ya taifa ya Brazili na klabu ya Paris Saint Germain Neymar amesema kuwa angependa kwenda kucheza nchini Marekani kwenye ligi ya Major League Soccer angalau kwa msimu mmoja kabla ya kustaafu kucheza mpira.

Neymar kwa sasa yuko na mkataba na klabu ya Paris saint Germain ambao unaisha juni 2025, ikiwa klabu yake ya sasa haitahitaji tena kumuongezea mkataba basi anaweza kutimkia MLS.

Neymar
Neymar

Wakati akihojiwa alisema kuwa anavutiwa zaidi kucheza marekani kuliko nchini mwake Brazil, alinukuliwa akisema.

“Sijui kama nitacheza tena Brazili, nina mashaka na hilo, ningependa kucheza Marekani, nimgependa kucheza pale angalau hata kwa msimu mmoja, kwanza kabisa wana msimu mfupi, kwaiyo ningekuwa na miezi mitatu ya likizo.

Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona alisema kuwa hajapanga ni wapi ambapo atatundika daluga, lakini alisema kuwa atacheza hadi mwisho wa mkataba wake kuisha kwenye klabu ya PSG.

“Nataniana na marafiki zangu kwamba nitastaafu nikiwa na miaka 32, lakini ni utani, sijui, kiukweli, nitacheza mpaka akili yangu itakapochoka, ikiwa akili yangu iko sawa na mwili uko vizuri, nadhani nina miaka michache ya kucheza, lakini afya ya akili ni kitu muhimu sana.

Neymar


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa