Mbappe Atuma Onyo Kwa Bayern Asema ‘’Real Madrid Ndio Wababe wa Ulaya’’

Nyota wa soka wa Ufaransa, Kylian Mbappé, ametuma kijembe kizito kuelekea mchezo wa robo fainali ya UEFA Champions League dhidi ya Bayern Munich utakaochezwa mwezi ujao, akionesha kujiamini kwa kiwango kikubwa.

Mbappe Atuma Onyo Kwa Bayern Asema ‘’Real Madrid Ndio Wababe wa Ulaya’’Mbappé amesisitiza kuwa licha ya Bayern Munich kuingia kwenye hatua hiyo wakiwa na kasi ya ajabu ya ushindi wa jumla ya mabao 10-2 dhidi ya Atalanta, bado anaamini nguvu ya Real Madrid haiwezi kubezwa kirahisi.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

“Wapo kwenye fomu bora kwa sasa, lakini kama kuna timu inaweza kuwafunga, ni Real Madrid,” amesema Mbappé, akionesha wazi imani yake kwa klabu hiyo ya Hispania inayojulikana kama Los Blancos.

Mbappe Atuma Onyo Kwa Bayern Asema ‘’Real Madrid Ndio Wababe wa Ulaya’’Mshambuliaji huyo ameendelea kuonesha ubora wake msimu huu wa Ligi ya Mabingwa, ambapo tayari amefunga mabao 13 katika mashindano hayo, akichangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya timu yake hatua kwa hatua.

Mbali na mafanikio ya Ulaya, Mbappé pia ameweka rekodi binafsi ya kuvutia kwa kufikisha karibu mabao 40 katika mashindano yote msimu huu, jambo linaloonyesha kiwango chake cha juu uwanjani.

Mbappe Atuma Onyo Kwa Bayern Asema ‘’Real Madrid Ndio Wababe wa Ulaya’’Aidha, nyota huyo amewahakikishia mashabiki kuwa bado yupo makini na majukumu yake, akisisitiza kuwa hajajiondoa katika ushindani kuelekea FIFA World Cup 2026, huku akiamini Real Madrid itaendelea kuthibitisha ubabe wake barani Ulaya baada ya kuitoa Manchester City kwa jumla ya mabao 5-1.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.