Marcus Rashford sasa anapitia kipindi cha mageuzi makubwa katika timu ya taifa ya England, kufuatia kutoshibidiwa kwake kwenye kikosi cha fainali za Euro 2024 na fomu isiyo thabiti katika mechi za hivi karibuni.
Tangu Thomas Tuchel achukue mikoba ya kuifundisha England, amempa Rashford imani kubwa, akisisitiza kuwa kasi na uwezo wake wa kipekee vinaweza kufungua milango katika mashindano ya Kombe la Dunia 2026. “Ninaona Rashford ana kila kitu kinachohitajika kuwa mchezaji wa msingi; anaweza kubadili kasi ya mchezo katika dakika yoyote,” alisema Tuchel.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Hata hivyo, mjadala mkubwa bado unazunguka upande wa kushoto kati ya Rashford na Anthony Gordon. Tuchel anatafuta mchezaji wa aina ya “safe-breaker,” ambaye anaweza kuleta kasi na hatari ya kufungia. Kwenye hoja hiyo, Rashford anaonekana kuwa kiongozi wa safu hiyo.
Takwimu za Rashford msimu wa 2025/26 zinaonyesha ukuaji wak, akiwa mkopo wa Barcelona, amefunga magoli 10 na kutoa assist 11 katika mashindano yote, huku akiwa na goli 5 katika Champions League, akitambulika miongoni mwa wachezaji hatari zaidi wa Barca Ulaya msimu huu.
Kwa upande wa timu ya taifa chini ya Tuchel , Rashford amefunga goli 1 katika mechi 7 za kufuzu Kombe la Dunia, jambo linaloonesha hatua yake ya kurejea kwenye kiwango cha juu. “Kila mechi ni fursa ya kuthibitisha nafasi yangu,” alisema Rashford baada ya mazoezi ya hivi karibuni.

