
De Bruyne aliipatia City goli la penati kwenye mchezo dhidi ya Liverpool dakika ya 25 baada ya Joe Gomez kumchezea madhambi Raheem Sterling,ambaye alifunga timu yake hiyo ya zamani goli la pili baada ya dakika kumi kupita.
Phil Foden aliweka kambani goli la tatu kabla ya Alex Oxlade-Chamberlain kujifuga goli la nne alipo jaribu kuzuia shuti la Sterling na kufanya Liverpool kulala kwa goli 4-0.
De bruyne alihusika kwenye magoli mawili na kiwango alichokionesha katika mchezo huo kimemfanya mwalimu wake Guardiola aweze kumtaja kama ndio kiungo wa kati bora kwa sasa ulimwenguni.
“Ni mchezaji mzuri sana, anakitu cha pekee katika soka lake,” Guardiola aliwaambia waandishi baada ya mchezo kumalizika.
“Anaweza akakimbia na kufungua macho yake kuangalia wachezaji wenzake, kiwango anacho kionesha kwa sasani kikubwa amefunga penati nne mfululizo kwenye nechi tulizo cheza.
“Kwa sasa katika nafsi ya kiungo ni bora kabisa.
“Ni kweli anaweza akawa bora zaidi. kivipi? Yeye anajua.”
Foden kwa mara nyigine ameweza kuwa na mchango mzuri katika mchezo huu, akiwa na timu ya Uingereza ya vijana wenye umri chini ya miaka 21 kiungo huyo amejihakikishia goli la nne katika michezo mitatu ya Premier League tangu ligi irejee.
“Tuna jitahidi kumlinda,” alisema Guardiola.
“Hatumchezeshi kila mechi, kwa wachezaji wadogo ni kuwa na umakini nao katika hatua za mwanzo.
“Ni mchezaji wa aina yake anafanya vitu ambavyo vinanishawishi kusema kwamba kwa siku za mbele atakua mchezaji wa kiwango cha juu sana.
Mchezaji mwenzake waliomaliza pamoja kwenye Academy Eric Garcia alirudi dimbani baada ya kupona maumivu aliyoyapta kwenye mchezo dhidi ya Arsenal ambapo City walishida kwa 3-0 na mchezo dhidi ya Liverpool alianza kama beki wakati.
“Amecheza dhidi ya Salah na Mane na ana umri wa miaka 19 tuu, alikuwepo kwenye mazoezi kwa siku tatu au nne baada ya kukaa nje kwa siku kumi na alicheza vizuri sana.

Eric Garcia na Phil Foden
“Kama timu tunajivunia kuwa na hawa vijana Phil na Eric tunawahesabu katika kikosi bila shaka.”



Mariam mtandama
Vizur
Dorophina
Guardiola yupo sahihi Kevin ameisaidia sana man city
Sadick
KDB ni kiungo bora kwa sasa ,hilo halina ubishi. Huwa najiuliza kwanini Chelsea ya Mourinho haikuona hilo#meridianbettz
Magdalena
Anachokisema guardiola ni Cha kweli kabisa
felister
Ni mchezaji mzuri sana ana kitu cha pekee kwny soka lake
Ester jackson
Pongezi sana timu ya Manchester city kwa kuonyesha mko vizuri mkizingatia mlikuwa na majeruhi lakini kijana mdogoahiri na matata Kevin De Bruyne aliweza kutamba sana uwashani na kuwashinda mabigwa wa Liverpool kwa magoli 4-0 mpaka ikampelekea mwalimu Guardiola aweze kumtaja kama ndio kiungo wa kati bora kwa sasa ulimwenguni inafurahisha sana kwa kweli .#meridianbettz
farida ahmadi
De bruyne ni kiungo mzuri Sana pia hameisaidia timu ya Manchester city kwa kiwango kikubwa Sana timu yake ni mchezaji mzuri Sana pia hata kweny timu yake ya taifa ya ubeligiji Yuko vizuri gardiola hajaongopa kabisah
Caroline
Kweli kabisa
Genia Sikaluzwe
Guardiola ni kiungo Bora anaejitabuwa na yupo sahihi
Lydia Emmanuel Magoti
Yah nivizuri akitoa kitu alicho kuwanacho moyoni kukipongeza nakukisifia Guardiola yupo sahii kuongea
Zeiyana
De bruyne ni mchezaji mzuri sana anakiatu cha kipekee katika soka lake la mpira pia hana mchango mkubwa sana man city kwa uwezo wake alio ufanya hanastairi pongezi sana
isha
Ni sahihi kabisa
Theckla
Ni mchezaji mzuri sana, anakitu cha pekee katika soka lake
Mwajuma
Lazima aseme hivyo kwa sababu nimchezaji wake
Revina
Kocha Guardiola anachosema yupo sahihi kabisa mchezaji wake sio wa mchezo mchezo mpambanaji na anajua anachokifanya
Antony Luseno
Hilo halina ubishi japo ni mchezaji asiyezungumziwa sana
lombo
hayo n maon yake
Hamidu
Tarent plaper#meridianbettz
Flomena
Ni mchezaji wa aina yake anafanya vitu ambavyo vinanishawishi kusema kwamba kwa siku za mbele atakua mchezaji wa kiwango cha juu sana.
Khadija
Yaaan lazima aongee hivo kwa sababu ni mchezaji wake#meridianbettz
Johnmary joel
Ninamkubali sana#meridianbett
Sylvester
De Bruyne sio kiungo bora tu duniani kwa sasa bali ni kiungo bora duniani anaeishi,uchezaji wake wa mpira ni moja kati ya viungo bora waliowahi kutokea duniani
Issa
Kiwango cha De brunye kwa sasa kipo juu na anajua kutawala sana kiungo ingawaje majeruhi yamekuwa yakimuandama hapo nyuma na kufanya city kuteteleka kidogo ila anaimudu nafasi na atakuwa bora sana
Kwa mbeleni
Gabriel
Habar njema sana 👍 kwa mkongwe huyo japo kashazeeka ila waswahil tunasema anazeeka vzur
Shafii
De brune ni mchezaji mzuri Sana hakuna asiyefahamu ilo kikubwa kwa msimu huu kilicho muangusha kupafomu vizuri ni majeraha ya Mara kwa Mara ila ni bonge la player
Njiku
Jamaa yupo poa licha ya pepe gardiola kuona kuwa de bruyne ni kiungo bora duniani jamaa anajituma na uchezaji wake ni wakipewa unaweza kumuweka popote na klabu yeyote akakupa matoke uchezaji wake anaweza cheza liverpool,buyern munich,real madrid na PSG kwa staili anayochezea me namfananisha na viungo ambao waliopita kama Paul school,frank lampard,Steven gerradi na alonso.de brunyne anacheza popote
warda
Ligi ikianza Tena Mambo yatakuwa matamu kinyama#Meridianbetz
Ernest
De Bruyne fundi sana
nasra
Safii
Hope mwaikuka
Nlkua cjui hii
Fatuma kasomo
Nimtazamo wake
Samiah
Nisawa kbs
Rehema
Big up
Furahav
Hongera brune.
Salma
Ni mchezaji mzuri
Saupha mohamed
Kweli kabsaa
Omary lukumbi
Kelvin de bruyne sio mbaya n fundi wa kibeljiam mzungu chuma ila sio top Middlefielder kuliko wote dunian ila kwa maoni ya pep yeye yuko sawa kwa upande wake
David Pere
Kwa maoni yake yeye
Latifa juma mohamed
Hakika ni kiungo Bora anayejitambua
Amani
KDB ni kiungo bora kwa sasa ,hilo halina ubishi.
Tatu
Ni sahihi kabisa
Povel
Kvd yupo vzr lkn tuwape muda wa kuwa vzr Zaid hv Sasa nmapema Sana kusema kafika ubora wa viungo waliopitah
Amiri Kayera
Maoni yake km Koch huwez mkataz ila kwang kuna walio mzd
Devotha
Asante sana
Sabrina
Maoni:De Bruyne yuko vizuri
Angelina
Guardiola yuko sahihi kabisa