Beki wa kushoto wa kimataifa wa Ureno Nuno Mendes amesaini mkataba wa miaka minne na klabu ya Paris Saint-Germain kwa kutumia kipengele cha kumnunua katika mkataba wa mkopo walikuwa nao awali.
Mendes mwenye umri wa miaka 19 alijiunga na PSG kwa mkopo akitokea klabu ya Sporting CP mwaka jana mabingwa hao wa Ligue 1 waliwasajili kwa uhamisho wa bure Lionel Messi na Sergio Ramos.
Uhamisho wa Mendes umegharimu kiasi cha €40m ambayo imeenda kwa Sporting CP ambapo sasa ataonyuesha zaidi uwezo wake huko Paris.
Mlinzi huyo wa kushoto amecheza michezo 37 kwenye mashindano yote ambapo 27 ni kutoka kwenye Ligue 1 akitengeneza nafasi 19 na kutoa asisti 1.
SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!


