Kocha Nasreedin Nabi wa Yanga amesema kuwa mipango iliyopo ni kuhahakisha wanashinda mchezo wao wa marudiano na Zalan FC ya Sudan kwenye hatua za awali za Ligi ya Mabingwa Afrika na kutinga kwa kishindo kwenye hatua ya kwanza.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Klabu ya Yanga Walter Harrison ambapo aliweka bayana kuwa mchezo huo wa pili ndiyo utakwenda kuamua kuwa wanakwenda hatua inayofuata au wataondoshwa, hivyo wanatakiwa kucheza kiume na mwalimu amekuwa akisistiza juu ya kupata mabao mapema.

Yanga, Yanga Wawapigia Hesabu Kali Zalan FC, Meridianbet

Walter alisema: “Kocha amekuwa akisisitiza juu ya wachezaji kutouchukulia poa mchezo huo kwa sababu labda tulishinda kwenye mechi ya kwanza. Mpira wa miguu haupo hivyo kabisa.

“Amewaambia wachezaji watambue umuhimu wa kushinda mchezo huo kwa hali yoyote kwa sababu ndiyo unakwenda kuamua kama tunasonga mbele au tunatolewa. Mikakati aliyoipanga ni mikubwa mno na ninaamini ushindi upo wa mapema sana.”

Yanga watacheza na Zalan FC kesho Jumamosi mchezo wa marudiano kwenye uwanja wa Mkapa, huku wakiwa tayari wanaongoza kwa mabao 4-0. Wanahitaji sare ya aina yoyote au ushindi ili wasonge mbele, huku Zalan wanatakiwa kushinda 5-0 ili wasonge mbele

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa