Kaizer Chiefs wamemtangaza Stuart Baxter kuwa kocha mpya wa timu hiyo akisaini kandarasi ya miaka miwili kuinoa timu hiyo yenye maskani yake Soweto.

Stuart Baxter (67) amewahi kuinoa Kaizer Chiefs kati ya mwaka 2012-2015 na alipata mafanikio ndani ya timu hiyo kwa kutwaa taji la Ligi kuu ya Africa Kusini mara mbili sambamba na kutwaa Nedbank Cup na MTN 8.

Stuart Baxter alifundisha Bafana katika vipindi viwili tofauti – kutoka 2004 hadi 2005 ‚na 2017 hadi 2019 – kuwaongoza kufika robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2019 huko Misri – lakini alishindwa kufuzu Kombe la Dunia la 2006 na 2018.

Kocha huyu Stuart Baxter amesafiri vizuri pia amefundisha huko Sweden ambapo alishinda taji la ligi na makombe mawili ya Svenska Cupen na AIK na Helsingborgs akiwa na Japan.

Huku akisaidiana na wasaidizi wake, Zwane na Sheppard waliongoza Chiefs kushinda 3-2 dhidi ya Golden Arrows na kushinda 1-0 dhidi ya TS Galaxy na kumaliza nafasi ya nane katika Ligi kuu ya PSL.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa