Mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi Matthijs De Light amethibitisha kuwa yupo kwenye mazungumzo ya kuaongeza mkataba na klabu ya Juventus, japokuwa hakuna makubaliano waliyofikiana mpaka sasa.

De Light mkataba wake na vibibi vya Turin unaisha June 2024, kuna taarifa nchini Italia zinasema mlinzi huyo yuko tayari kusaini kuongeza mwaka mmoja mbele kwenye mkataba wake, ikiwa ada ya kuvunja mkataba itapunguzwa kutoka ya sasa €125milion hadi kufikia  €70milion

De Light

“Bado tupo kwenye mazungumzo, lakini sio sababu kwamba ndio tayari tuna makubaliano, kama ilivyoandikwa.” De Light alisema.

“Sio kweli. Makubaliano bado yanaendelea lakini bado yapo kwenye hatua za mwanzo. Bado nina miaka miwili kwenye mkataba wangu, kwaiyo bado nina muda wa kutosha kabisa”

De Ligt alijiunga na klabu ya Juventus akitokea Ajax kwa uhamisho wenye thamani €85m kwenye majira ya kiangazi mwaka 2019. Mkataba wake na  Bianconeri unaisha mwaka  June 2024.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa