kiungo wa Simba Jonas Mkude amesema kuwa haikuwa kazi rahisi kushinda mbele ya Tanzania Prisons kutokana na ugumu wa timu hiyo kwenye mchezo wao wa ligi kuu uliochezwa jana uwanja wa Sokoine Mbeya.

Mkude alipachika bao la ushindi kwenye mchezo huo na kuwapa ushindi huo wa kwanza kwa Simba mbele ya Prisons baada ya muda mrefu upite tangu walipofanya hivyo wakiwa wanacheza ugenini.

Mkude, Mkude: Haikuwa Rahisi Kuwafunga Tanzania Prisons, Meridianbet

Mkude alisema baada ya mchezo huo kuwa: “Kucheza na Tanzania Prisons kunahitaji kujipanga na timu ambayo itapata nafasi inaweza kushinda hivyo tulifanya maandalizi mazuri na tulipambana kusaka ushindi.”

Ni bao la kwanza la Mkude kwenye ligi msimu wa 2022/23 akiwa na uzi wa Simba.
Pia ni mchezo wa kwanza kwa Kocha Mkuu, Juma Mgunda kushuhudia wakipata pointi tatu kwenye mchezo wa ligi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa