Baada ya kuwa na mwenendo usioridhisha, Uongozi wa Kagera Sugar umeweka wazi kuwa, kikosi kwa sasa kitabaki Jijini Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Singida Big Stars .

Mchezo huo wa raundi ya tano inatarajiwa kupigwa Septemba 27 katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Kagera Sugar, Kagera Sugar Bado Inajipanga!, Meridianbet

Ofisa Habari wa kagera Sugar, Hamis Mzanzala amesema: “Kikosi kinaendelea vizuri japokuwa mchezaji wetu Deogratius Mafie anaendelea na matibabu baada ya kupata majeraha mazoezini kabla ya kuanza Kwa Ligi Kuu hivyo alilazimika kwenda kufanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini.

“Tutaendelea kubaki Jijini Mwanza, kwaajili ya maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Singida Big Stars.

“Kocha wetu Mkuu, Francis Baraza pamoja na benchi lake la ufundi wanaendelea kufanya maboresho yote ya mapungufu na makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo wetu uliopita, ili tufanikiwe kufanya vizuri na kupata alama tatu mbele ya Singida.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa