Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji, raia wa Marekani, Melis Medo ameahidi kuwa mpaka kufikia mwisho wa msimu huu timu hiyo itakuwa nafasi ya sita au ya saba kwenye msimamo wa ligi.
Medo tangu aanze kukinoa kikosi cha Dodoma Jiji jana jumanne alifanikiwa kupata ushindi wa kwanza kwenye ligi dhidi ya KMC.
Akizungumza baada ya kuibuka na ushindi huo wa mabao 2-1 dhidi ya KMC, Medo alisema: “Ni kweli umekuwa mchezo wangu wa kwanza kupata ushindi tangu nianze kukinoa kikosi.
“Nimebadilisha vitu vingi sana tangu nianze kuinoa timu kuanzia aina ya uchezaji pamoja na falsafa hivyo tulistahili kupata ushindi wa leo.
“Mpaka kufikia mwisho wa msimu huu tutakuwa kwenye nafasi ya sita au ya saba katika msimamo wa ligi.”