Straika wa Azam FC, Idriss Mbombo ameonekana kuwa mtambo wa mabao ndani ya klabu hiyo baada ya kufunga bao la sita.
Bao hilo pekee lilifungwa jana jumanne kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Mbombo ameifungia Azam bao hilo pekee na kufanikiwa kufikisha mabao sita kwenye ligi kuu akiwa mfungaji wa pili katika msimamo wa wafungaji.
Baada ya ushindi huo Azam wamefikisha pointi 26 wakiwa wamecheza michezo 12 huku kwa sasa wakiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi.