Clement Mzinze nyota wa Yanga aliyezima ndoto za Kagera Sugar ya Mecky Maxime kutibua rekodi ya timu hiyo kutofungwa ni dereva bodaboda na fundi ujenzi.
Nyota huyo alifunga bao pekee ubao wa Uwanja wa CCM Kirumba uliposoma Kagera Sugar 0-1 Yanga dakika ya 18 akitumia pasi ya Feisal Salum.
Mshambuliaji huyo amesema: “Nimezaliwa Tanga nina miaka 18, nikaenda Iringa kufanya kazi za ujenzi nikaacha nikafanya kazi ya bodaboda nilikuwa ninafanya kazi hizo huku ninacheza mpira.
“Mimi ni mshambuliaji kufunga bao lazima ujiskie vizuri.Kwanza nilipoona nimeanza nilishikwa na hofu, mechi yangu ya kwanza, hali ya hewa ilikuwa ngumu kidogo.
“Namshukuru Mungu wachezaji wenzangu walinipa moyo na kuniambia kwamba ni lazima nicheze kwa kujiamini ninaweza, nisiwe na mtetemo ikiwa ni pamoja na Sure Boy, Kibwana, Sure Boy,Mwamnyeto, sikuwa na hofu yoyote.
“Kuna watu watatu niliwaambia kwamba ninaanza wakae kwenye kideo na wote waliniambia kwamba nitafunga goli na iliwezekana ikiwa ni pamoja na Hyrat ambaye aliniambia nitafunga huyu ni rafiki yangu zawadi ya goli hili ninampa yeye.
“Mwalimu aliniambia kwamba ikiwa Mayele atakuwa amerudi nyuma mimi lazima niende mbele n ahata pasi ilipokuwa inapigwa Mayele aliniambia nirudi eneo ambalo niliambiwa niwe hivyo amekuwa ni mshauri wangu pia ninamkubali ninajifunza vingi kwake,”.