Siku ya kesho Jumatano Yanga wanatarajia kushuka dimbani kucheza na Club Africain wakiwa ugenini na mashabiki wengi wakiwa na hofu ya timu yao kupenya, hali ni tofauti kwa wachezaji wa timu hiyo kwa mujibu wa nahodha Bakari Mwamnyeto.

Bakari alisema, wao kama wachezaji wameshafanya vikao vingi wakiwa Tunisia kuelekea kwenye mchezo huo na kubwa walikuwea wakipeana moyo na kutiana nguvu na kujua kuwa mchezo huo ni kama michezo mingine ila wanatakiwa kuwa na lengo moja hilo la kutusua.

Mwamnyeto, Mwamnyeto: Club Africain Hawasumbui, Tunajiamini, Meridianbet

Mwamnyeto alisema: “Tunajua kuwa mashabiki wanahofu na mchezo huu kuna ambao wanajua kuwa tutafungwa mabao mengi sana. Lakini niwaambie tu sisi kama wachezaji hatuna hofu na tunakwenda kwenye mchezo huu tukiwa na nia moja ya kufuzu.

“Wachezaji wakubwa na wale wenye uzoefu na michezo kama hii hasa kwenye nchi hii walikuwa wanatumia muda wao kwenye vikao vyao kuwapa moyo na kuwafanya waone huu mchezo wa kawaida.

“Mimi nilishawahi kucheza kwenye huu mchezo hapa Tunisia kwenye uwanja huu na kweli kuna mashabiki wengi. Lakini kwetu haitusumbui kwa sababu hata mechi za Simba na Yanga huwa na mashabiki wengi.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa