Simba Queens wanatarajia kushuka dimbani kesho Jumatano kucheza mechi ya nusu fainali na mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita Mamelody Sundowns kutoka Kanda ya Cosafa na Afrika Kusini.

Simba watashuka dimbani kucheza mchezo huo kwenye mji wa Rabat saa 11 jioni ikiwa ni mara ya kwanza wanafika kwenye hatua hiyo. Simba walikusanya alama sita kwenye kundi A nyuma ya AS Far.

Simba Queens, Simba Queens Kufa au Kupona Kesho, Meridianbet
Mchezo mwingine wa nusu fainali hiyo ni kati ya majirani wa Tanzania TP Mazembe kutoka DR Congo, ambao watacheza na AS Far saa 4 usiku wa leo.

Kocha wa Simba, Charles Alex Lukula alisema kuwa: “Hatuna cha kupoteza kwenye mchezo huo, ingawaje kila mmoja wetu anajua kuwa tunakwenda kukutana na timu bora na bingwa wa mashindano haya.

“Tutajitolea kwa kila namna sisi kama makocha kuhakikisha tunawakumbusha vijana kuwa umuhimu wa kushinda mechi hii ni mkubwa sana.”

Opah Clemant, nahodha wa timu hiyo aliliambia Championi Jumatano kuwa: “Sisi tupo tayari kwa mchezo huo ambao unakwenda kuwa mgumu. Tupo tayari kwa kila kitu na ninaimani tunakwenda kushinda.”

Simba hawana cha kupoteza kwenye mchezo huo kwa kuwa wameshafikia kwenye malengo waliyojiwekea ya kutinga kwenye nusu fainali na wanacheza mchezo huo kama ni zaidi ya matarajio waliyofikia.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa