Klabu ya Simba inatarajia kushuka dimbani leo kwa Mkapa kukiwasha dhidi ya Horoya kwenye mchezo wao wa ligi ya Mabingwa barani Afrika huku kila timu ikihitaji kufuzu hatua ya robo fainali.
Mchezo huo utapigwa majira ya saa 1:00 usiku hii leo katika dimba la Benjamin Mkapa ambapo ni pointi tatu tu ambazo zitagombaniwa leo. ODDS KUBWA unazipata ndani ya Meridianbet.
Simba kwenye mchezo wa kwanza walipokutana, alipoteza kwa bao 1-0 ugenini na hii leo amekuja na kaulimbiu inayosema kuwa “Tunaitaka Fainali” ambayo amekuja nayo Afisa habari wa klabu hiyo Ahmed Ally.
Kaulimbiu hiyo ni kwaajili ya kuhamasisha wachezaji kucheza kwa ari lakini pia mashabiki kujaa uwanjani kwaajili ya kuitazama timu yao inafanya vizuri na kupata matokeo yatakayowawezesha kwenda hatua inayofuata.
Horoya inashikilia nafasi ya tatu wakati mnyama yeye anashikilia nafasi ya pili hivyo kutokana na msimamo jinsi ulivyo kila timu kama ikipata matokeo kwenye mechi mbili zizlizobaki inaweza kwenda robo fainali.