Simba SC, imemtangaza Clatous Chama kuwa mchezaji bora kwa mwezi Agosti kwa kupata kura nyingi kutoka kwa mashabiki.

Kiungo huyo ameanza kwa kasi msimu wa 2022/23 ambapo kwenye mechi mbili za ligi kafunga bao moja katoa pasi moja ya bao na kasababisha faulo moja iliyoleta bao ilikuwa kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Geita Gold, Simba Sc iliposhinda mabao 3-0.

Chama atwaa tuzo ya Mchezaji Bora Simba SC
Chama

Taarifa rasmi iliyotolewa na klabu yake imeeleza namna hii: “Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki (Emirate Aluminium Simba Profile Fans Player of the Month) kwa mwezi Agosti, 2022 inakwenda kwa Clatous Chama,”.

Chama atwaa tuzo ya Mchezaji Bora Simba SC
Chama jr

Baada ya ujumbe huo Chama alidondosha ujumbe wake kwa kusema “Asante sana simba mmejua kuniheshimisha,”.

Wachezaji ambao amewashinda ni Sadio Kanoute na Pape Sakho wote ni viungo ndani ya klabu hiyo iliyokuwa inanolewa na Kocha Mkuu, Zoran Maki kabla ya kufikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuachana na klabu hiyo leo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa